Uturuki imesema inatafuta kushirikiana na Zambia katika kukuza usimamizi endelevu wa maji na usafi wa mazingira.
Balozi wa Uturuki nchini Zambia, Huseyin Barbaros Dicle, alitoa kauli hiyo jijini Lusaka Jumanne baada ya kukutana na Waziri wa Maendeleo ya Maji na Usafi wa Mazingira, Collins Nzovu.
"Tulikuwa na mkutano wenye tija na mheshimiwa Collins Nzovu, Waziri wa Maendeleo ya Maji na Usafi wa Mazingira. Tulijadili masuala ya ushirikiano katika sekta ya usimamizi endelevu wa maji na usafi wa mazingira," alisema Dicle.
Nzovu alismhukuru Dicle kwa ziara hiyo na akaeleza kuwa Zambia inatarajia msaada wa Uturuki katika kukuza teknolojia inayolenga kuboresha mbinu za kuhifadhi maji.
Nchi hiyo ya kusini mwa Afrika inajikakamua kutokana na ukame mkali wa msimu wa 2023/2024 na sasa inatafuta kutumia mbinu kama ya kuhifadhi maji kama njia ya usimamizi endelevu wa maji.