‘Harambee Stars’ imesonga mbele kwenye michuano hiyo baada ya DRC kuifunga Angola kwa mabao 2-0, na hapo awali Morocco kuichabanga Zambia magoli 3-1, katika mechi zilizochezwa Agosti 14.
Iwapo watafungwa na Zambia katika mchezo huo, basi watashuka hadi nafasi ya pili ya kundi A, na kujiwekea uwezekano mkubwa wa kukutana na ‘Taifa Stars’ ya Tanzania, ambayo iliingia hatia ya 8 bora, wakiwa na alama zao 9.
Mechi hiyo inasuburiwa kwa hamu sana, hasa ukizingatia upinzani wa jadi ulioko kati ya Tanzania na Kenya, hasa katika masuala mbalimbali kama vile kisiasa, kiuchumi na hata kitamaduni.
Kwa mfano, si ajabu kuona wakitofautiana hoja kuhusu hali za kisiasa na kiuchumi baina ya nchi hizo mbili, utajiri wa maliasili na hata wakati mwingine, kupimana ubavu kwenye uwezo wa kuzungumza lugha ya Kiswahili na Kiingereza.