21 Agosti 2025
Licha ya ahadi lukuki za fedha na mambo mengine kutoka kwa viongozi wa nchi hizo tatu kwa wachezaji na mabenchi ya ufundi ya nchi hizo, mashabiki waliofurika katika viwanja vya Benjamini Mkapa wa Dar es Salaam, Moi Kasarani pale Nairobi na Mandela uliopo jijini Kampala, walikuwa ni hamasa na motisha kubwa kwa wachezaji hao, walipokuwa wakitoa machozi, jasho na damu kupigania bendera na fahari za nchi zao.
Kwa sasa, mashabiki hao tunaweza kuwaita mchezaji wa 12 wa Tanzania, Kenya na Uganda, na pengine tunaweza kuwaona tena uwanjani, iwapo timu hizo zikiweza hatua ya nusu fainali na fainali.