19 Agosti 2025
Tanzania inakabiliwa na mtihani mgumu wakati itakapovaana na Morocco katika mchezo wa robo fainali ya michuano ya CHAN 2024, utakaofanyika Agosti 22, 2025.
Mara ya mwisho Tanzania kuifunga Morocco, ilikuwa ni mwaka 2013, katika mchezo wa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia.
Ikiongozwa na Mdenmark Kim Poulsen, ‘Taifa Stars’ ilishinda mabao 3-1, yakitiwa kimiani na Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu.