13 Agosti 2025
Unaweza kuita vita ya Daudi na Goliath, au kisa cha Sisimizi kumuua Tembo.Hicho ndicho kilichotokea usiku wa Agosti 12, baada ya timu ya taifa ya Sudan kuushangaza ulimwengu kwa kuifunga Nigeria mabao 4-0 katika mechi ya Kundi D ya michuano ya CHAN 2024.
Nigeria, ambayo inafahamika kwa kutoa wachezaji nyota ulimwenguni na kufanya vizuri kimataifa, inashika nafasi ya 44 duniani, kwa mujibu wa viwango vya ubora wa soka, vilivyotolewa na FIFA mwezi Julai mwaka huu.
Kwa upande wake, Sudan, taifa ambalo linakabiliwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa muda mrefu sasa, inashika nafasi ya 110 duniani, kulingana na orodha ya FIFA.