Aliyewahi kugombea nafasi ya urais nchini DRC mwaka 2023 Rex Kazadi, amejiunga rasmi na kikundi cha waasi cha AFC/M23.
Kazadi ameripotiwa kujiunga na vuguvugu hilo Machi 30, 2025.

Shutuma hizo zinakuja wiki moja baada ya Bisimwa kudai kuwa vijiji vinavyokaliwa na jamii ya Banyamulenge vilikuwa vikishambuliwa na majeshi ya serikali ya DRC.
“Nina furaha sana kuwa mwanachama wa Alliance Fleuve Congo siku ya leo,” alisiskika Kazadi katika picha mjongeo iliyonaswa kutoka katika mkutano na waandishi wa habari.
“Ahsanteni sana kwa kunipokea kwa dhati, hakika ni heshima kubwa kuwa sehemu yenu. Niko tayari kusaidia kufikia malengo yetu.”
Uamuzi wake unakuja saa chache baada ya mratibu wa AFC/M23 Corneille Nangaa kuwataka raia wa DRC waishio ughaibuni kujiunga na vuguvugu hilo ili kuiokomboa nchi hiyo.
Wakati akizindua kampeni yake ya uchaguzi jijini Kinshasa mwaka 2023, Kazadi aliahidi kusaidia mchakato wa upatikanaji amani katika eneo la Mashariki mwa DRC.