10 Juni 2025
Uingereza imewawekea vikwazo mawaziri wawili wa Israeli wa siasa za mrengo wa kulia kwa matamshi yao kuhusu Gaza, vyombo vya habari viliripoti siku ya Jumanne.
Waziri wa Usalama Itamar Ben-Gvir na Waziri wa Fedha Bezalel Smotrich watakabiliwa na marufuku ya kusafiri na mali zao zitapigwa tanchi kama sehemu ya hatua zilizotangazwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza David Lammy.
Wawili hao "walichochea vurugu za misimamo mikali na ukiukwaji wa haki za binadamu za Wapalestina," alisema Lammy, kama ilivyoripotiwa na shirika la habari la BBC.
Kwa mujibu wa taarifa, wakijibu kuhusu vikwazo hivyo, Israeli imesema "ni makosa sana kwa wawakilishi waliochaguliwa na watu na maafisa wa serikali kuchukuliwa hatua za aina hii."