Rais wa Syria Ahmed al Sharaa ametangaza makubaliano ya dharura, na kusema kuwa nchi hiyo imepokea wito wa kimataifa kuingilia kati mzozo wa ndani katika mji wa Sweida na kurejesha usalama katika eneo hilo.
"Matukio ya hivi majuzi katika jimbo la Sweida yameashiria mabadiliko ya hatari, na mapigano makali kati ya makundi haya yangeweza kutokomea kudhibitiwa kama taifa la Syria halingeingilia kati kutuliza hali," al Sharaa alisema wakati wa hotuba ya televisheni siku ya Jumamosi.
Pia alibainisha kuwa si haki kulaani jamii nzima ya Druze kwa matendo ya watu wachache.
"Druze ni sehemu ya msingi ya vita vya Syria, kutengwa kwao ni tishio la moja kwa moja kwa utulivu wa Syria," Rais Sharaa alisema.
Uchokozi wa Israel
"Watu wa Sweida wanasimama kidete na serikali, isipokuwa kwa wachache," alibainisha, akiongeza kuwa serikali "inakataa mauaji na ukiukwaji wote uliofanyika ..." katika jimbo hilo.
Pia alitoa shukrani kwa makabila ya wenyeji kwa misimamo yao ya kishujaa na kuwataka kusitisha mapigano kabisa.
Rais al Sharaa pia alihutubia mashambulizi ya Israel kusini na Damascus ambayo yalilenga taasisi za kimkakati za serikali na vikosi vya ndani.
Uchokozi wa Israel "umefufua tena mvutano na kuipeleka nchi hiyo katika hatua ya hatari ambayo inatishia uthabiti wake kutokana na mashambulizi ya wazi ya mabomu ya kusini na taasisi za serikali huko Damascus," Sharaa alibainisha.
Heshimu mapatano
Al Sharaa alionya kwamba Syria haitakuwa uwanja wa vita kwa malengo ya kujitenga au miradi iliyogawanyika.
Rais wa Syria pia alishukuru Uturuki, Marekani na nchi za Kiarabu kwa msaada wao kwa Damascus katika awamu hii.
Mapema siku hiyo, ofisi ya Rais Ahmed al Sharaa ilitangaza "kusitisha mapigano mara moja" huko Sweida siku ya Jumamosi wakati vikosi vya Wizara ya Mambo ya Ndani vikitumwa katika jimbo lenye watu wengi wa Druze chini ya makubaliano na Israel.
Ofisi ya rais ilitoa wito kwa "wahusika wote kuheshimu kikamilifu" mapatano hayo, ambayo yalikuja baada ya Israel kushambulia kwa mabomu vikosi vya Wizara ya Ulinzi vilivyotumwa katika jimbo hilo la kusini mapema wiki hii kulazimisha kujiondoa.
Vikosi maalum kwa Sweida
Vikosi vya usalama vya Syria vilianza kutumwa katika jimbo la kusini la Sweida siku ya Jumamosi kufuatia siku za mapigano makali na machafuko, Wizara ya Mambo ya Ndani imesema.
"Kufuatia matukio ya umwagaji damu yaliyosababishwa na makundi haramu, na chini ya amri ya moja kwa moja kutoka kwa Urais, vikosi vya usalama vya ndani vimeanza kutumwa Suwayda kama sehemu ya ujumbe wa kitaifa," msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani Noureddin al Baba alisema katika taarifa yake Jumamosi.
Al Baba aliongeza kuwa "lengo lao kuu ni kuwalinda raia na kumaliza machafuko," akiongeza kuwa "vikosi vya usalama vitatumia rasilimali zao zote kukomesha mashambulizi, kumaliza mapigano, na kurejesha utulivu katika jimbo hilo."
Kauli hiyo imekuja saa chache baada ya balozi wa Marekani nchini Uturuki kusema Syria na Israel zilikubaliana kusitisha mapigano.
Mapignao kati ya Druze na Bidouin
Mnamo Julai 13, mapigano yalizuka kati ya makabila ya Waarabu wa Bedouin na vikundi vilivyojihami vya Druze huko Sweida.
Ghasia ziliongezeka na mashambulizi ya anga ya Israeli yakafuata, ikiwa ni pamoja na maeneo ya kijeshi ya Syria na miundombinu huko Damascus.
Israel ilitaja "ulinzi wa jamii za Druze" kama kisingizio cha mashambulizi yake.