AFRIKA
1 dk kusoma
Sudan imeripoti maambukizi 1,300 ya kipindupindu na vifo 18 katika wiki moja
Wizara ya afya ya Sudan imeripoti maambukizi mapya ya kipindupindu, huku idadi hiyo ikifika 1,307 na vifo 18 vilivyosababishwa na ugonjwa huo ndani ya wiki moja.
Sudan imeripoti maambukizi 1,300 ya kipindupindu na vifo 18 katika wiki moja
Mlipuko wa kipindupindu, ambao umeua makumi ya watu, ulitangazwa nchini Sudan mnamo Agosti 2024. /Picha: / Reuters
22 Julai 2025

Katika taarifa yake Jumanne, wizara hiyo ilisema maambukizi hayo yalirekodiwa katika majimbo 12 kati ya 18 ya Sudan kati ya Julai 12 na 18, na kuongeza jumla ya maambukizi tangu kuanza kwa mlipuko wa Agosti 2024 hadi maambukizo 91,034, pamoja na vifo 2,302 katika majimbo 17.

Idadi kubwa zaidi ya maambukizi wiki jana ilirekodiwa huko Tawila, Darfur Kaskazini, ikiwa na maambukizi 519, ikifuatiwa na maambukizi 236 huko Qeissan, Jimbo la Blue Nile.

Kwa kulinganisha, wizara iliripoti maambukizi 674 vya kipindupindu na vifo 13 wiki iliyotangulia, kati ya Julai 5 na 11.

Kuporomoka kwa miundombinu ya Sudan

Mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu unaoendelea umeenda sambamba na kuporomoka kwa miundombinu ya Sudan kutokana na mapigano kati ya jeshi na kikosi RSF.

Jeshi na RSF wamekuwa wakipigana vita tangu Aprili 2023 ambavyo vimeua zaidi ya watu 20,000 na wengine milioni 14 kuyahama makazi yao, kulingana na makadirio ya Umojwa wa Mataifa na mamlaka za mitaa.

Utafiti kutoka vyuo vikuu vya Marekani, hata hivyo, unakadiria idadi ya vifo kuwa karibu 130,000.

InayohusianaTRT Global - Wakimbizi wa Sudan wanapambana na kipindupindu huku WHO ikionya kuenea hadi kambi za Chad
CHANZO:AA
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us