14 Agosti 2025
Toka atangazwe kuionoa ‘Harambee Stars’ mwezi wa tatu mwaka huu, ni wazi kuwa Benedict Saul McCarthy ameleta mabadiliko makubwa ndani ya kikosi hicho, ndani ya muda mfupi, tofauti na ilivyokuwa kwa watangulizi wake.
Ni ukweli usiopingika kuwa, nyota huyo wa zamani wa Porto ya Ureno, ameongeza ari ya ushindani na kujiamini ndani ya kikosi cha ‘Harambee Stars’.
Katika michezo saba aliyoiongoza timu ya taifa ya Kenya, McCarthy ameisadia timu hiyo kushinda 3, kutoa droo 3 na kupoteza mchezo mmoja tu dhidi ya Gabon, na hivyo kurudisha matumaini ya mashabiki wa ‘Harambee Stars’ kwa timu yao ya taifa.
Wingi wa mashabiki wanaojaza uwanja wa Moi Kasarani, ni ushahidi tosha wa imani kubwa waliyonayo kwa McCarthy na kikosi chake.