12 Agosti 2025
Ikiwa tayari imejikusanyia alama 7 baada ya michezo mitatu, ‘Harambee Stars’ ni kama vile ipo mguu ndani, mguu nje kutinga robo fainali.
Uganda wanahitaji suluhu ya aina yoyote kwenye mchezo wao wa mwisho dhidi ya Afrika Kusini yenye alama 3, wakiombea Guinea ifungwe na Algeria kwenye mchezo wa Agosti 18.
Timu ya DRC bado wana nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali, kufuatia ushindi wao wa mabao 2-0 dhidi ya Zambia, Agosti 7.