Waziri wa Mambo ya Nje Hakan Fidan na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio wamezungumza kwa njia ya simu na kujadilia juhudi za kidiplomasia zinazoendelea kumaliza vita vya Ukraine,pamoja na yanayojiri nchini Syria na Gaza, kulingana na vyanzo vya kidiplomasia.
Mazungumzo hayo ya Jumanne yanakuja siku moja baada ya Uturuki kuwa wenyeji wa hatua ya pili ya mazungumzo ya amani ya wajumbe kati ya Urusi na Ukraine jijini Istanbul.
Urusi na Ukraine walikubaliana kubadilishana wafungwa zaidi wakiangazia wenye mahitaji muhimu —watoto na wale ambao wamejeruhiwa vibaya —na kueleza nia ya kurejesha miili ya wanajeshi 6,000 waliouawa katika kila upande.
Majadiliano mapana ya kikanda
Pamoja na Ukraine, Fidan na Rubio walibadilishana mawazo kuhusu hali ya hatari inayozidi kwa watu wa Gaza na kuendelea kwa hali tete nchini Syria.
Hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa, lakini vyanzo vya Uturuki vimeeleza mazungumzo hayo kama "muhimu" na "yanayoendelea."
Mkutano wa Jumatatu ulikuwa ni hatua ya pili ya juhudi za upatanisho jijini Istanbul,kufuatia mazungumzo ya awali ya 16 Mei. Huku ikiwa bado mapigano hayajasitishwa, waangalizi wanaona kuwa kubadilishana wafungwa na kurejeshwa kwa miili ya waliouawa vitani kama hatua ndogo lakini muhimu katika kumaliza uhasama.
Uturuki inafahamika kama mpatanishi wa migogoro, kuendeleza ushirikiano wa kidiplomasia na wote Ukraine na Urusi.
Marekani, huku ikiwaunga mkono Ukraine kijeshi na kidiplomasia, imeunga mkono juhudi zinazolenga kuhakikisha hali inakuwa sawa kwa raia na majadiliano.