AFRIKA
1 dk kusoma
Polisi aliyempiga risasi muuzaji barakoa Nairobi akamatwa – Ripoti ya polisi
Afisa wa polisi aliyempiga risasi raia aliyekuwa akiuza barakoa wakati wa maandamano yaliyofanyika jijini Nairobi mnamo Juni 17, 2025, amekamatwa. Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na msemaji wa Polisi, Muchiri Nyaga.
Polisi aliyempiga risasi muuzaji barakoa Nairobi akamatwa – Ripoti ya polisi
Muathiriwa yuko hospitalini apokea matibabu kulingana na ripoti ya polisi- ripoti ya polisi. /Picha: Citizen Digital / Other
17 Juni 2025

“Kufuatia tukio hilo, Inspekta Jenerali wa Huduma ya Kitaifa ya Polisi ameagiza kukamatwa kwa afisa aliyehusika, kuanzishwa kwa uchunguzi wa haraka, na kufikishwa kwake mahakamani. Afisa huyo tayari amekamatwa,” ripoti hio ilisema .

Maandamano hayo, ambayo yalikuwa na lengo la kushinikiza kujiuzulu kwa Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Eliud Lagat, yaligeuka na kuwa ya vurugu baada ya makundi ya wahuni kuwavamia waandamanaji.

Ripoti hiyo pia ilibainisha kuwa muathiriwa wa tukio hilo alipelekwa hospitalini ambapo anaendelea kupokea matibabu.

Katika mojawapo ya video zilizosambaa mtandaoni na kuibua taharuki miongoni mwa wananchi, maafisa wawili wa kikosi cha kupambana na ghasia walionekana wakimkamata muuzaji huyo wa barakoa, kumshambulia, na hatimaye kumpiga risasi.

Ripoti zinaonyesha kuwa magenge ya watu waliokuwa wamejihami waliwashambulia waandamanaji kwa kuwapiga na kuwaibia, hali iliyochangia machafuko hayo kuenea.

Taarifa ya polisi ililaani vikali vitendo hivyo vya kihalifu na kusisitiza kuwa watu wote waliotenda uhalifu wakati wa maandamano hayo watachukuliwa hatua kali za kisheria.

“Watu wanaojihusisha na vitendo vya kihuni watakabiliwa kwa uthabiti kwa mujibu wa sheria. Uchunguzi wa kina umeanzishwa ili kuwabaini na kuwachukulia hatua za kisheria wanaohusika,” taarifa hiyo iliendelea.

InayohusianaTRT Global - Mtu mmoja auawa katika maandamano Kenya - ripoti
CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us