ULIMWENGU
2 dk kusoma
Kiongozi wa kanisa Katoliki ataka amani Sudan na Nigeria
Takriban watu 200 waliuawa kikatili huko Yelwata, katika eneo la Serikali ya Mtaa ya Guma nchini Nigeria usiku wa tarehe 13 na 14 Juni, 2025.
Kiongozi wa kanisa Katoliki ataka amani Sudan na Nigeria
Papa Leo VIV ameombea amani Nigeria na Sudan / picha: @CatholicSat / Public domain
15 Juni 2025

Kiongozi wa kanisa Katoliki Papa Leo XIV alifanya ibada spesheli Jumapili kwa ajili ya wahanga wa "mauaji mabaya" katika Jimbo la Benue, Nigeria.

Takriban watu 200 waliuawa kikatili huko Yelwata, katika eneo la Serikali ya Mtaa ya Guma usiku wa tarehe 13/14 Juni.

Wengi wao wakiwa wakimbizi wa ndani waliopewa makao na kanisa Katoliki".

Akizungumza katika ibada Jumapili Papa aliombea "usalama, haki, na amani" nchini Nigeria, akiongeza kuwa alikuwa anawatakia mema hasa "jumuiya za Kikristo za vijijini za Jimbo la Benue ambao wamekuwa wahanga wa ghasia".

Shirika la Amnesty International Nigeria siku ya Jumamosi lilitoa wito kwa mamlaka ya Nigeria "kukomesha mara moja umwagaji damu unaokaribia kila siku katika Jimbo la Benue na kuwafikisha wahusika halisi mbele ya sheria".

Mzozo wa Sudan

Papa leo pia aliongelea Sudan, ambayo imekuwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa zaidi ya miaka miwili.

Papa Leo alisema aliarifiwa kuhusu kifo cha Padre Luke Jumu, paroko wa El Fasher kusini-magharibi mwa nchi hiyo, ambaye anaripotiwa kuuawa katika shambulio la hivi majuzi.

"Wakati ninatoa maombi yangu kwa ajili yake na waathiriwa wote, narudia wito wangu kwa wapiganaji kuacha uhasama, kulinda raia, na kuanza njia ya mazungumzo kwa ajili ya amani." Papa alisema.

Kisha akahimiza jumuiya ya kimataifa kuongeza juhudi zake za kutoa misaada ya kibinadamu kwa idadi ya watu ambayo "imeathiriwa sana" na mgogoro unaoendelea.

CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us