ULIMWENGU
2 dk kusoma
Erdogan, bin Salman wajadiliana kuhusu hali tete ya Israeli na Iran katika mazungumzo ya simu
Rais wa Uturuki ameonya kuwa kanda hiyo haiwezi kuhimili tena mzozo mwingine, akisisitiza vita kamili vitasababisha idadi kubwa ya watu kuhama kwenda sehemu zingine.
Erdogan, bin Salman wajadiliana kuhusu hali tete ya Israeli na Iran katika mazungumzo ya simu
Rais wa Uturuki Erdogan anasema mashambulizi ya Israeli kwa Iran ni jaribio la kutibua juhudi za amani. / AA
14 Juni 2025

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman kujadili hali tete ya usalama kati ya Israeli na Iran, pamoja na masuala ya kikanda na dunia, kulingana na taarifa kutoka kwa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Uturuki.

Wakati wa mazungumzo hayo siku ya Jumamosi, Rais Erdogan alionya kuwa Israeli, chini ya uongozi wa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, ni "hatari kubwa kwa uthabiti na usalama katika kanda hiyo".

Alisema ameonesha hilo kwa mara nyingine kupitia mashambulizi ya hivi sasa dhidi ya Iran.

Erdogan alisisitiza kuwa Israeli lazima iache kuchochea uhasama. Pia aliilaumu jamii ya kimataifa "kwa kutokemea suala la kukaliwa kwa Palestina pamoja na mauaji ya halaiki", akisema kuwa kunyamazia hilo kunawapa Israeli kiburi cha kutekeleza "ukiukwaji wa sheria na vurugu".

Pia rais wa Uturuki alisema mashambulizi ya Israeli kwa Iran—huku kukiwa na mazungumzo ya upatanishi kati ya Marekani na Iran—ilikuwa ni njia moja ya kutibua juhudi za amani.

Mashambulizi hayo, alisema, yamesababisha sialaha za nyuklia kuvuja na kwa mara nyingine kuonesha namna IsraelI "inatishia amani ya kanda na dunia".

Erdogan ameonya kuwa kanda hiyo haiwezi kuhimili mzozo mwingine, akisisitiza kuwa vita zaidi vitasababisha watu kuhama kutoka sehemu moja hadi nyingine na kwamba matatizo ya nyuklia yanatakiwa kutatuliwa kwa njia ya majadiliano yanayoendelea.

CHANZO:TRT World
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us