Wizara ya Maji na Nishati ya Ethiopia imesema Bwawa la Grand Ethiopian Renaissance (GERD) lilizalisha megawati 6,800 za nishati ya umeme katika kipindi cha miezi tisa iliyopita, huku mitambo mitano ikifanya kazi kwa sasa.
Ujenzi wa bwawa la GERD ulianza mwaka 2011 katika mto Nile.
Habtamu Itefa, Waziri wa Maji na Nishati, aliviambia vyombo vya habari vya serikali kuwa bwawa hilo "limefikia awamu yake ya mwisho" na sasa lina uwezo wa "kuhifadhi kiasi kikubwa cha maji."
Alisema kuwa kila moja ya mitambo mitano inayofanya kazi inazalisha megawati 400.
GERD hatimaye inapanga kuwa na mitambo 11.
Katika kipindi kama hiki mwaka jana, Nishati ya Umeme ya Ethiopia (EEP) iliripoti kuwa GERD ilizalisha zaidi ya saa 2,700 za gigawati za umeme kwa kutumia turbine mbili, kila moja ikiwa na uwezo wa karibu megawati 375.
Shirika lilionyesha kuwa pato hili liliwakilisha asilimia 16 ya jumla ya uzalishaji wa umeme nchini wa 16,900 za gigawati katika kipindi cha miezi kumi mnamo 2023.
EEP pia ilikadiria kuwa, mara tu baada ya kukamilika, bwawa la GERD litaongeza uwezo wa uzalishaji wa nchi kwa asilimia 83.
Kwa mujibu wa shirika hilo, bwawa hilo linatarajiwa kufikia uwezo wa kuzalisha megawati 5,150 na kuzalisha wastani wa saa 15,760 za umeme kila mwaka.
Mwezi Machi 2025, Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed aliwaambia wabunge nchini humo kuwa itazindua Bwawa la Grand Ethiopian Renaissance (GERD) ndani ya miezi sita.
Bwawa hili ambalo ni rasilimali muhimu ya nisgati barani Afrika, limefadhiliwa na wananchi wa Ethiopia bila kutegemea misaada au mikopo kutoka nje, kwa hiyo nchi hiyo inalichukulia kama fahari yake kubwa.