AFRIKA
2 DK KUSOMA
WFP linasitisha shughuli zake zote nchini Sudan huku mapigano yakiendelea
Shirika la chakula la Umoja wa Mataifa linasema usalama wa wafanyakazi wake wa misaada ya kibinadamu huku kukiwa na mapigano mapya nchini Sudan ndio kipaumbele chao kikuu
WFP linasitisha shughuli zake zote nchini Sudan huku mapigano yakiendelea
WFP Sudan | Picha: Reuters / Reuters
16 Aprili 2023

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, linasema ndege moja inayosimamiwa na WFP iliharibiwa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Khartoum wakati wa mapigano ya risasi tarehe 15 Aprili.

Mapigano makali yamezuka kati ya Jeshi la Sudan na Vikosi vya Rapid Support Forces, RSF.

Katika taarifa yake Mkurugenzi Mtendaji wa WFP, Cindy McCain anasema wafanyakazi watatu wa WFP waliuawa Jumamosi tarehe 15 Aprili katika ghasia huko Kabkabia, Darfur Kaskazini walipokuwa kikazi. Wengine wawili walijeruhiwa katika tukio hio.

"Wakati tunapitia hali inayoendelea, tunalazimika kusitisha kwa muda shughuli zote nchini Sudan," anasema MCCain.

Kusimamisha shughuli za WFP kutaathiri takriban watu milioni 18; milioni 3 ambao ni wakimbizi wa ndani, na inakadiriwa watu milioni 15 ambao WFP inasema wanakabiliwa na uhaba wa chakula.

Shirika la UNHCR linasema Sudan inawahifadhi takriban wakimbizi milioni 1.1, wengi wao wanatoka nchi jirani ya Sudan Kusini. Wengine kutoka Eritrea na Ethiopia.

"WFP imejitolea kusaidia watu wa Sudan wanaokabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula, lakini hatuwezi kufanya kazi yetu ya kuokoa maisha ikiwa usalama na usalama wa timu na washirika wetu haujahakikishwa,"

WFP inauliza Jeshi la Sudan na Vikosi vya Msaada wa Haraka vya kijeshi, kufikia makubaliano ambayo yatahakikisha usalama wa wafanyakazi wa kibinadamu nchini.

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us