UTURUKI
2 dk kusoma
Israel inanufaika na mgawanyiko wa Syria: Fidan
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Hakan Fidan, amesema kwamba Israel inanufaika na mgawanyiko wa Syria na inatamani hali hiyo ya kukata tamaa iendelee.
Israel inanufaika na mgawanyiko wa Syria: Fidan
Israel inanufaika na mgawanyiko wa Syria na inatamani kuwe na hali ya kukata tamaa. /
25 Julai 2025

Katika mahojiano na vyombo vya habari vya ndani, Fidan alisema:

"Ninaamini kuwa utawala wa Sharaa umejibu matarajio ya eneo na jumuiya ya kimataifa licha ya kuwa na rasilimali chache."

Akizungumzia nafasi ya Marekani katika Syria na eneo hilo kwa ujumla, Fidan alisema kwamba, mbali na uhusiano maalum wa Marekani na Israel, Marekani imekuwa na mchango chanya katika eneo hilo.

Kuhusu ushirikiano wa kiulinzi na Syria, alisema Uturuki siku zote imeunga mkono ushirikiano wa halali katika sekta hiyo.

Mapema wiki hii, Fidan alionya kuwa iwapo makundi ndani ya Syria yataelekea kwenye mgawanyiko na hali ya kutokuwa na utulivu, Uturuki itachukulia hilo kama tishio la moja kwa moja kwa usalama wake wa taifa na itaingilia kati.

Alisisitiza kuwa Ankara iko tayari kwa mazungumzo na kushughulikia madai ya makundi hayo, mradi tu hayahusishi mgawanyiko wa nchi hiyo.

"Israel inaendesha sera ya kuudhoofisha ukanda wake na kuendeleza machafuko," alisema, akiongeza kuwa Israel haitaki kuona nchi yoyote katika eneo lake ikiwa thabiti, na inalenga kuigawa Syria.

Fidan alisema Uturuki inafuatilia kwa karibu maendeleo katika eneo la kusini mwa Syria, yaliyozuka kufuatia kuingilia kwa Israel.

Wakati jumuiya ya kimataifa na wadau wa kikanda wanajitahidi kuhakikisha Syria haigeuki kuwa eneo salama la magaidi au chanzo cha uhamiaji usiodhibitiwa, Israel – kwa mujibu wa Fidan – inajitahidi kuhujumu juhudi zote za kuleta amani, utulivu na usalama nchini humo.

Akitamatisha, Fidan alisisitiza kuwa Uturuki imekuwa ikifanya juhudi kubwa kwa muda mrefu kumaliza migogoro na vita katika eneo hilo, na akathibitisha tena dhamira ya nchi hiyo kupitia mikakati ya kidiplomasia.

CHANZO:TRT World and Agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us