Mfumo wa malipo wa serikali ya Ghana umeongezeka kutokana na idadi ya ‘‘wafanyakazi hewa 67,311 ," na kusababisha kuwepo kwa juhudi za kuokoa dola milioni 14,398,861, anasema Waziri Fedha Cassiel Ato Forson.
Akizungumza katika bunge la nchi hiyo wakati wa kutathmini bajeti ya nusu mwaka ya 2025 siku ya Alhamisi, Dkt. Forson alibaini kuwa Ukaguzi wa Hesabu za serikali Ghana zimebaini matatizo aina mbili.
"Wafanyakazi 14,000 ambao hawajulikani na wafanyakazi 53,311 ambao pengine wamestaafu, kujiuzulu, wamefutwa kazi, wako likizo bila malipo au wamekufa, na bado wako kwenye mfumo wa malipo ya serikali."
Shirika la habari la Ghana limeripoti kuwa waziri ametoa onyo kwa wale waliohusika na ubadhirifu huo.
Fedha za umma
“Acha nitumie fursa hii kuwaonya vikali wale waliohusika “wafanyakazi hewa” kote katika utumishi wa umma kuwa tutawawajibisha mmoja mmoja kwa kupotea kwa fedha za umma ,” alieleza.
Forson alieleza bunge kuwa ukaguzi utakamilika kufikia mwisho wa mwezi Agosti 2025, na umma utafahamishwa kuhusu “yaliyogunduliwa na matokeo.”