AFRIKA
2 dk kusoma
Wakimbizi wa DRC na Rwanda kurejea nyumbani kwa hiari
DRC, Rwanda na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) walifanya mkutano wa ngazi ya juu wa mawaziri wa pande tatu nchini Ethiopia na kukubaliana juu ya kurejea nyumbani kwa wakimbizi wa nchi hizo mbili kwa hiari.
Wakimbizi wa DRC na Rwanda kurejea nyumbani kwa hiari
Mawaziri wa rwnda na DRC wamekubalian kuwa wakimbizi kwa nchi zao warejee makwao kwa amani/ Picha: @RwandaEmergency / Public domain
25 Julai 2025

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) lilifanya mkutano wa ngazi ya juu wa mawaziri wa pande tatu nchini Ethiopia siku ya Alhamisi kujadili kurejea kwa hiari kwa wakimbizi, wa Jamhuri ya kidemokrais ya Congo DRC na Rwanda.

DRC na Rwanda zilisaini makubaliano ya pamoja.

InayohusianaTRT Global - Umoja wa Afrika wapongeza makubaliano ya amani kati ya DRC na Rwanda kama 'hatua muhimu'

Tamko hilo la pamoja lilitiwa saini na Waziri wa Mambo ya Ndani wa DRC, Jacquemain Shabani, Balozi wa Rwanda Charles Karamba na Kamishna Mkuu Msaidizi wa Operesheni wa UNHCR Raouf Mazou.

Pande hizo zilipitisha muongozo wa kati ya 2025 na 2026 kuhusu ‘Kurejesha Makwao kwa Hiari na Kuunganishwa tena kwa Hiari,’ ikionyesha hatua muhimu, majukumu, na ratiba za matukio, kufuatia kazi ya maandalizi katika mkutano wa kikundi huko Addis Ababa mnamo Julai 22-23.

Mikutano hiyo ilifuatia makubaliano ya amani ya Washington ya Juni 27 kati ya DRC na Rwanda na azimio la Julai 19 la Doha kati ya DRC na waasi wa M23.

'Mahitaji ya wakimbizi wa ndani yanapaswa kuzingatiwa'

Kundi la waasi la M23, kitovu cha mzozo wa mashariki mwa DRC, linadhibiti eneo kubwa, ikiwa ni pamoja na miji mikuu ya majimbo ya Goma na Bukavu, ambalo liliteka mapema mwaka huu.

Pande hizo tatu ziliahidi kuharakisha kuwarejesha makwao wakimbizi 600 wa Rwanda walioko Goma, kuimarisha mashauriano ya jamii, kuchunguza ushiriki ili kurejesha matarajiao ya amani chini ya Azimio la Doha la Julai 2025, na kujitolea katika mipango jumuishi ya kuwawezesha kurudi nyumbani tena.

Walisisitiza kuwa mpango endelevu wa kurudisha wakimbizi ni muhimu kwa amani, utulivu, na ahueni baada ya vita, hasa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na eneo la Maziwa Makuu.

"Katika muktadha huu, hali na mahitaji ya wakimbizi wa ndani pia yanapaswa kuzingatiwa," taarifa hiyo ilionyesha.

Ujenzi wa amani na utulivu wa kikanda

Walitambua jukumu la UNHCR kama "mtendaji asiyeegemea upande wowote," aliyepewa jukumu la kutoa ulinzi na kutafuta suluhisho la kudumu kwa wakimbizi.

Pande hizo zilithibitisha kujitolea kwao kwa kurejea kwa hiari, salama, na kwa heshima kama msingi wa suluhu ya kudumu, inayochangia katika ujenzi wa amani na utulivu wa kikanda.

Walikubali kufanya mikutano ya wataalamu ya mara kwa mara chini ya Utaratibu wa Utatu na kukutana tena katika ngazi ya mawaziri katika muda wa miezi sita ili kutathmini maendeleo na kutoa mwongozo.

CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us