UTURUKI
4 dk kusoma
Kampuni ya Uturuki ya kutengeneza makombora, Rokestan, yasaini mikataba ya kikmkakati ya ulinzi
Kampuni ya Roketsan yavutia mashirika mengi katika maonesho ya ulinzi ya IDEF kwa bidhaa zake bunifu.
Kampuni ya Uturuki ya kutengeneza makombora, Rokestan, yasaini mikataba ya kikmkakati ya ulinzi
Roketsan iliwavutia sana waliohudhuria maonyesho hayo na bidhaa zake za ubunifu na mifumo iliyothibitishwa uwanjani. /
24 Julai 2025

Kampuni ya kutengeneza makombora ya Uturuki, Roketsan, imesaini mikataba mipya ya ushirikiano wa kimkakati wa ndani na nje ya nchi katika Maonesho ya Kimataifa ya Sekta ya Ulinzi (IDEF) 2025 yanayoendelea mjini Istanbul.

 Toleo la 17 la maonesho hayo ya siku sita lililoanza Jumanne, linafanyika kwa wakati mmoja katika Kituo cha Maonesho cha Istanbul, Uwanja wa Ndege wa Ataturk, Hoteli ya Wow, na Atakoy Marina.

Tukio hilo limeandaliwa na KFA Fairs kwa usaidizi kutoka Sekretarieti ya Viwanda vya Ulinzi ya Uturuki (SSB) na Mfuko wa Vikosi vya Ulinzi vya Uturuki, huku Anadolu akiwa mshirika wa mawasiliano wa kimataifa.

 Roketsan ilivutia washiriki wengi kwa bidhaa zake za ubunifu na mifumo iliyokwisha kuthibitishwa katika nyanja mbalimbali, na kuifanya kuwa moja ya kampuni mashuhuri zaidi katika maonesho hayo.

Kampuni hiyo ilikamilisha mikataba muhimu inayohusiana na usambazaji wa bidhaa na miradi mipya katika hafla za utiaji saini zilizofanyika siku mbili za kwanza za maonesho.

Ushirikiano wa mifumo ya mizinga na Azerbaijan

Roketsan iliimarisha ushirikiano wake wa kimkakati na Azerbaijan katika sekta ya ulinzi kwa kusaini protokali mpya ya ushirikiano wa mifumo ya mizinga.

Protokali hiyo, iliyojulikana kama "Artillery Systems Cooperation Protocol," ilianza kutumika Julai 22, na ilisainiwa na Naibu Waziri wa Ulinzi wa Azerbaijan, Agil Gurbanov, na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Roketsan, Faruk Yigit.

InayohusianaTRT Global - Uturuki yadhibiti hatua muhimu ya ulinzi kwa kuzindua kombora la hypersonic katika maonesho ya IDEF

Makubaliano ya kihistoria ya mradi wa Gokbora

Mkataba wa uendelezaji wa mradi wa kombora la Gokbora Beyond Visual Range la anga kwa anga, ambao ulianzishwa mnamo IDEF 2025, pia ulitiwa saini Jumatano kati ya Sekretarieti ya Viwanda vya Ulinzi (SSB) na Roketsan.

Mkataba huo ulitiwa saini na Rais wa SSB Haluk Gorgun na Meneja Mkuu wa Roketsan Murat Ikinci.

Gokbora, ambayo itatumiwa na ndege za kivita za kuendeshwa na rubani na zisizo na rubani, imepangwa kuwa nguvu mpya ya jeshi la anga yenye safu yake ya maili 100 za baharini na uwezo wa juu zaidi wa uongozi.

Zaidi ya hayo, mkataba ulitiwa saini kati ya Roketsan na kampuni nyingine ya ulinzi ya Uturuki ya Aselsan kwa ajili ya kuendeleza vichwa vya RF na mifumo midogo ya kuunganisha data iliyopachikwa kwa makombora chini ya mradi huo.

Mikataba ya kimkakati na SSB

Roketsan na SSB walitia saini mikataba miwili muhimu. Mkataba wa Mradi wa Mfumo Mchanganyiko wa Makombora/Makombora ya Roketi na Protokoli ya Ushirikiano wa Usambazaji wa Mfumo wa Kombora la TRLG-122.

Mikataba hii inalenga kuendeleza na kununua mifumo muhimu itakayoinua uwezo wa ulinzi wa Uturuki.

Roketsan na kampuni nyingine ya ulinzi ya Uturuki, MKE, pia walisaini mkataba wa usambazaji wa vijiti vya nishati (fuel rods) vitakavyotumika katika miradi mbalimbali.

Mkataba huo ulisainiwa na Meneja Mkuu wa Roketsan, Murat İkinci, na Meneja Mkuu wa MKE, İlhami Keleş.

Roketsan ilisaini protokoli nyingine mpya na Teknopark Istanbul ili kusaidia ubunifu na maendeleo ya biashara changa katika sekta ya ulinzi na teknolojia.

Protokoli hiyo, iitwayo “Protokoli ya Ushirikiano wa Kimkakati kwa Kituo cha Kukuza Ubunifu (Incubation Center),” ilisainiwa na Murat İkinci na Mkurugenzi Mkuu wa Teknopark Istanbul, Abdurrahman Akyol.

Ushirikiano huu unalenga kuibua mawazo bunifu, kusaidia biashara changa (startups), na kuchangia kwenye mfumo wa ikolojia katika sekta ya ulinzi.

Jitihada za utengenezaji wa ndani

Siku ya Alhamisi Julai 24, Roketsan ilisaini Makubaliano ya Maelewano kuhusu Jitihada za Kitaifa na kampuni ambazo imekuwa ikishirikiana nazo hadi sasa: Armsto Konnektor, Asil Çelik, Sensorsan Sensor Technologies, İveo Electronic Defence Systems, Korel Elektronik, na Pavezyum Kimya.

Jukwaa la Roketsan “Rise for Tomorrow”, lililozinduliwa mwaka jana, linachukua nafasi muhimu katika mpango huu wa uzalishaji wa ndani.

Jukwaa hili liliundwa ili kuongeza ufanisi wa juhudi za kitaifa, kuimarisha mahusiano na wasambazaji na kupunguza utegemezi wa nchi za nje katika mnyororo wa ugavi.

 Halid Bulut alisema kuwa ni muhimu kwa Roketsan kuendeleza juhudi za ndani ya nchi bila kupungua kasi, ili kupunguza utegemezi wa nje na kuongeza uhuru wa kiusalama wa kitaifa.

CHANZO:AA
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us