Nyota huyo wa mieleka ambaye jina lake halisi ni Terry Gene Bollea alianza mieleka ya kulipwa mwaka 1977 lakini akapata umaarufu zaidi alipojiunga na WWF kabla ya kubadilisha jina na kuwa WWE mwaka 1983.
Mkongwe huyo ambaye alikuwa na mtindo mahsusi wa nywele na masharubu yake alikuwa furaha ya mashabiki wengine kote duniani.
Kwa sisi vijana wa zamani tukipendelea kujiita Hulk Hogan pale tunapotaka kuonesha ubabe.
Alipenda pia kujifunga kitambaa cha kichwa au ‘bandana’ akiongeza na mbwembwe zake wakati anapoingia ulingoni.
Moja ya mbwembwe zake maarufu ni pale anapochana fulana yake kuonesha kama mtu aliyelishwa pufya na yuko tayari ‘kumchana’ mpinzani wake.
Kulikuwa na enzi za ‘Hulkamania’ ambapo katika pambano lake la kwanza la WWF la uzani wa juu mwaka 1984 alimshinda Iron Sheik.
Mmoja wa wale waliotuma salamu zao za rambirambi kutokana na msiba wa Hulk Hogan ni aliyekuwa hasimu wake ulingoni Undertaker.
Alishinda ubingwa wa WWE mara sita na amejumuishwa katika orodha ya wakongwe wa WWE 2005. Baadhi ya wapinzani wa Hulk Hogan ulingoni walikuwa Dwayne 'The Rock' Johnson, 'Macho Man' Randy Savage na Andre The Giant.
Baadaye alianza vipindi vyake mwenyewe.