AFRIKA
2 dk kusoma
Utapiamlo bado changamoto Somalia
Takwimu za mashirika ya kibinadamu zinaonyesha kuwa uhaba wa chakula utazidi kuwa mbaya katika miezi ijayo katika sehemu za Somalia huku takriban watoto 47,000 wanatarajiwa kuathiriwa na utapiamlo mkali.
Utapiamlo bado changamoto Somalia
Utapiamlo bado ni changamoto katika sehemu tofauti nchini Somalia/ Picha: ICRC / Public domain
12 Juni 2025

Shirika la Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) linaonya kuwa utapiamlo mkubwa miongoni mwa watoto umeenea kote nchini Somalia, huku vituo vya afya vinavyosaidiwa na shirika hilo vikishuhudia idadi kubwa ya waliolazwa tangu ukame wa miaka miwili iliyopita.

“Mwezi Mei pekee, kituo cha msaada katika Hospitali Kuu ya Kismayo kililaza watoto 277 waliokuwa wagonjwa mahututi, idadi kubwa zaidi ya mwezi tangu 2023. Kati ya Januari na Mei, kituo kililaza wagonjwa 863, ongezeko la takriban asilimia 70 ikilinganishwa na miezi mitano iliyopita,” ICRC imesema.

Vituo vya afya kama vile vilivyoko Kismayo vinatoa matibabu ya kuokoa maisha kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano ambao wanaugua matatizo ya kiafya yanayoletwa na njaa. Lakini ICRC inasema vifaa hivyo ni haba.

“Kliniki za lishe ambazo hapo awali zilikuwa na jukumu muhimu katika kuzuia utapiamlo zilifungwa kutokana na kupunguzwa kwa ufadhili, na kuziacha familia zilizo hatarini bila kupata huduma ya mapema,” ICRC imessema.

"Migogoro inang'oa familia, mafuriko yanaharibu mazao, na baadhi ya maeneo tayari yameharibiwa na ukame," alisema Antoine Grand, mkuu wa ujumbe wa ICRC nchini Somalia.

"Wazazi hawawezi kumudu chakula, na watoto wadogo ndio wa kwanza kufa kwa njaa."

Takwimu za mashirika ya kibinadamu zinaonyesha kuwa uhaba wa chakula utazidi katika miezi ijayo, huku takriban watoto 47,000 wakiathiriwa na utapiamlo mkali.

CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us