AFRIKA
2 DK KUSOMA
Shirika la ujasusi la Uturuki MIT limemkata makali gaidi mkuu wa PKK kaskazini mwa Iraq
Sebahat Ormanli, anayejulikana kwa jina la Mizgin Guyi, alipanga shughuli za kigaidi zinazohusisha uchomaji moto katika maeneo ya mijini na uchochezi wa moto wa misitu huko Uturuki.
Shirika la ujasusi la Uturuki MIT limemkata makali gaidi mkuu wa PKK kaskazini mwa Iraq
Ormanli has been actively involved in PKK's terrorist activities in Iraq's Sulaymaniyah region since 2022. / Others
14 Desemba 2023

Shirika la Kitaifa la Ujasusi la Uturuki (MIT) limefanikiwa kumkata makali gaidi Sebahat Ormanli, kwa jina la Mizgin Guyi, anayedaiwa kuwa mtu wa cheo cha juu ndani ya muundo wa vijana wa kundi la kigaidi la PKK.

Akiwa kiongozi wa Jumuiya ya vijana wanawake ya PKK (KJCK) na mmoja wa wanachama wake 18, Ormanli alitambuliwa kaskazini mwa Iraq kufuatia uchunguzi wa kina, duru za usalama za Uturuki zilisema Alhamisi.

Gaidi Ormanli alipatikana akipanga shughuli, ikiwa ni pamoja na kuchochea uchomaji moto wa misitu Uturuki na kuandaa uchomaji moto katika maeneo ya mijini, kama maagizo kwa wanachama wa KJCK.

Aliwekwa katika Orodha ya Wanaotafutwa ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya ya Uturuki chini ya kitengo cha Kijani.

Baada ya uamuzi wa kufanya operesheni hiyo, MIT, maafisa walipata mahali alipo Ormanli na walifanikiwa kumkata makali gaidi huyo wakati akiwa katika usafiri.

Akifanya kazi chini ya jina la Mizgin Guyi, Sebahat Ormanli aliwahi kuwa msemaji wa Jumuiya ya Vijana ya PKK huko Silopi, Sirnak, mnamo 2011.

Alijiunga na makada wa kijijini wa shirika la kigaidi mwaka 2012, baadaye alihamia Syria baada ya kuvuka kuelekea kaskazini mwa Iraq.

Huko, alichukua nafasi ya mtu anayehusika na muundo wa vijana wa kikundi cha kigaidi.

Tangu 2022, amekuwa akishiriki kikamilifu katika shughuli za kigaidi za PKK katika eneo la Sulaymaniyah nchini Iraq.

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us