AFRIKA
2 DK KUSOMA
Malawi yatangaza siku 21 za maombolezo ya kifo cha Makamu wa Rais
Maombelezo hayo yanaanza Juni 11 mpaka Julai 1, Baraza la Mawaziri la nchi hiyo limesema katika taarifa yake ya Jumanne.
Malawi yatangaza siku 21 za maombolezo ya kifo cha Makamu wa Rais
Wanandugu wa waathirika wa ajali hiyo walikuwepo kwenye uwanja wa ndege wa mjini Lilongwe kupokea miili ya wapendwa wao. Picha/Serikali ya Malawi / Others
12 Juni 2024

Malawi imetangaza siku 21 za maombolezo kufuatia kifo cha Makamu wa Rais wa nchi hiyo Saulos Chilima na watu wengine nane kwa ajali ya ndege.

Siku ya Jumatatu, Chilima na ujumbe wake walikuwa safarini kuelekea kaskazini mwa nchi hiyo kabla ndege ya kijeshi waliyoabiri kupoteza mawasiliano na rada kutokana na hali mbaya ya hewa.

Mabaki ya ndege hiyo yalipatikana siku ya Jumanne, ndani ya msitu mnene wa wenye vilima vikali karibu na mji wa Mzuzu.

Kipindi cha maombolezo kinaanza Juni 11 mpaka Julai 1, Baraza la Mawaziri la nchi hiyo limesema katika taarifa yake ya Jumanne.

Bendera kupepea nusu mlingoti

Rais Lazarus Chakwera ameelekeza bendera zote kupepea nusu mlingoti wakati wote wa maombolezo, iliongeza taarifa hiyo.

Kulingana na baraza hilo, taratibu za mazishi zitatangazwa hapo baadaye.

Mabaki ya miili ya Chilima na waathirika wengine ilisafirishwa kwa ndege kuelekea mji mkuu wa nchi hiyo, Lilongwe.

Rais Chakwera aliambatana na viongozi wengine wa serikali kuipokea miili hiyo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kamuzu, jumanne jioni.

Baadhi ya viongozi mbalimbali ulimwenguni wameendelea kutuma salamu zao za rambirambi kwa familia na serikali ya Malawi.

Pata habari zaidi kupitia whatsapp channels

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us