UTURUKI
2 DK KUSOMA
Mkuu wa maendeleo endelevu wa UN aunga mkono mpango wa Uturuki wa taka sifuri
Azimio la 'Global Zero Waste' taka sifuri, lililozinduliwa katika Mkutano Mkuu wa 78 wa Umoja wa Mataifa, linalenga kuendeleza mbinu endelevu duniani kote.
Mkuu wa maendeleo endelevu wa UN aunga mkono mpango wa Uturuki wa taka sifuri
Azimio la Global Zero Waste, lililozinduliwa katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa mwaka jana, linalenga kukuza mbinu endelevu duniani kote./ Picha: AA / Others
23 Septemba 2024

Jeffrey Sachs, rais wa Mtandao wa Suluhu Endelevu wa Umoja wa Mataifa, ametia saini Azimio la Nia Njema la 'Global Zero Waste' taka sufuri, baada ya kukutana na Mke wa Rais wa Uturuki Emine Erdogan mjini New York.

Mkutano huo ulifanyika Jumatatu katika Nyumba ya Uturuki wakati wa ziara ya Erdogan kwa Mkutano Mkuu wa 79 wa Umoja wa Mataifa.

Sachs alisifu uongozi wa Erdogan kwenye mradi wa taka sifuri. Sachs pia aliangazia mchango unaoweza kutolewa kupitia mtandao wake mwenyewe, unaojumuisha vyuo vikuu 2,000 katika nchi 150.

Pia alipongeza juhudi za upatanishi za Uturuki katika migogoro ya kimataifa, kama vile Ukraine, akibainisha kuwa amani ni muhimu kwa maendeleo endelevu.

Wito wa hatua ya pamoja ya kimataifa

Azimio la 'Global Zero Waste', lililozinduliwa katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa mwaka jana, linalenga kukuza mbini endelevu duniani kote.

Erdogan alionyesha shukrani kwa usaidizi wa Sachs, akisisitiza maono yao ya pamoja ya ulimwengu safi na endelevu zaidi.

Kupitia mtandao wa kijamii, Erdogan alisisitiza umuhimu wa mipango ya taka sifuri katika kuharakisha maendeleo kuelekea kufikia malengo ya maendeleo endelevu na kutoa wito wa hatua za pamoja za kimataifa kuelekea mustakbali wa haki na jumuishi.

Mnamo 2023, Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alijitolea kwa mpango wa taka sufuri kwa kutia saini azimio hilo.

Pata habari zaidi kupitia whatsapp channels

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us