AFRIKA
2 dk kusoma
Bajeti mpya ya Rwanda yalenga uwanja mpya wa ndege
Spika wa Baraza la Manaibu, Mbunge Gertrude Kazarwa, alisema kuwa muswada wa fedha za serikali utachunguzwa na kamati ya bunge inayowajibika - kabla ya kupigiwa kura kuwa sheria.
Bajeti mpya ya Rwanda yalenga uwanja mpya wa ndege
Waziri wa fedha wa Rwnda Yusuf  Murangwa, amesema mwaka huu nchi hiyo itazingatia ujenzi wa uwanja mpya wa ndege/ Picha Reuters
13 Juni 2025

Serikali ya Rwanda katika bajeti yake ya mwaka wa 2025/2026 inapanga kutenga takriban dola milioni 600 (takriban Rwf850 bilioni) ili kuharakisha ujenzi wa uwanja mpya wa ndege wa kimataifa huko Bugesera.

Waziri wa Fedha na Mipango ya Uchumi, Yusuf Murangwa amesema mgao huu unawakilisha takriban asilimia 70 ya pendekezo la ongezeko la matumizi ya zaidi ya dola milioni 840 ( takriban trilioni Rwf 1.2 katika mwaka ujao wa fedha ikilinganishwa na wa sasa).

"Mradi mmoja mkubwa ambao uko katika bajeti hii ni uharakishwaji wa Uwanja wa Ndege Mpya wa Kimataifa wa Kigali ulioko Bugesera. Tumekuwa katika mipango ya miundo kwa muda mrefu, tumekuwa katika shughuli za awali kwa muda mrefu," alisema.

Waziri huyo ameongezea kuwa lengo ni kukamilisha uwanja huo ifikapo 2028.

"Pia tuna wabia, ambao ni Qatar... Katika kupanga, tunaangalia karibu dola milioni 600, lakini utekelezaji utatueleza hasa jinsi utakavyotekelezwa na ushirikiano tulionao," alisema.

Murangwa ametoa maelezo hayo baada ya kuwasilisha muswada wa sheria ya bajeti ya mwaka 2025/26 Bungeni 12 Juni 2025.

Bunge liliidhinisha umuhimu wa muswada huo ambapo serikali inapanga kutumia zaidi ya dola bilioni 4/9 ( Rwf trilioni 7 ) katika bajeti ya kitaifa ya 2025/2026.

Kiasi hiki kinawakilisha ongezeko la zaidi ya dola milioni 840 (Rwf1.2 trilioni) ikilinganishwa na zaidi ya dola bilioni 4 (Rwf5.8 trilioni) iliyoidhinishwa kwa mwaka wa sasa wa fedha.

Spika wa Baraza la Manaibu, Mbunge Gertrude Kazarwa, alisema kuwa muswada wa fedha za serikali utachunguzwa na kamati ya bunge inayowajibika - kabla ya kupigiwa kura kuwa sheria.

Murangwa pia alitaja upanuzi wa kampuni ya ndege ya taifa ya RwandAir miongoni mwa miradi mikubwa ambayo serikali inalenga kutekeleza katika mwaka ujao wa fedha.

Uwanja wa ndege na RwandAir ni ubia kati ya serikali na Mamlaka ya Uwekezaji ya Qatar, ambapo serikali ya Rwanda itachangia asilimia 40 na asilimia 59 ya hisa katika uwanja wa ndege na shirika la ndege, mtawalia, kulingana na Wizara ya Fedha na Mipango ya Kiuchumi (MNECOFIN).

Bajeti ya 2025/2026

Ruzuku inatarajiwa kuwa zaidi ya dola laki 410 (bilioni 585), huku mikopo ya nje ikikadiriwa kuwa zaidi ya dola bilioni ¼ ( trilioni 2.1) Hii ni asilimia 30 ya jumla ya matumizi yaliyopendekezwa.

Kiasi cha mkopo wa nje kulingana na bajeti ni zaidi ya dola milioni 450 (Rwf648.4 bilioni).

CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us