27 Februari 2025
Mji Mkongwe ni eneo linalobeba historia kubwa ya Zanzibar, na linatambulika kama Eneo la Urithi wa Dunia wa UNESCO.
Mji Mkongwe unafanana na jumba la makumbusho lililo wazi lenye mitaa nyembamba, masoko ya rangi nyingi na usanifu wa kuvutia.
Utaratibu wa kila siku wa wenyeji, maandalizi ya asubuhi ya wavuvi na uchangamfu wa wachuuzi wa mitaani huvutia umakini wa watalii wanaotembelea kisiwa hichi .