AFRIKA
2 dk kusoma
UN yaonya kuhusu kuendelea kwa mzozo mashariki mwa DRC
Tangu mwanzoni mwa Mei, mapigano katika jimbo hilo tayari yalikuwa yamewalazimisha zaidi ya watu 12,000 kutafuta hifadhi katika kambi ya wahamiaji ya Rhoe, kilomita 70 kaskazini mwa mji mkuu wa jimbo la Bunia.
UN yaonya kuhusu kuendelea kwa mzozo mashariki mwa DRC
Mpango wa Mahitaji ya Kibinadamu wa dola bilioni 2.5 kwa DRC unafadhiliwa kwa asilimia 11 tu/ Picha: UNOCHA / Public domain
4 Juni 2025

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu, UN OCHA, inaripoti kuwa kuendelea kwa ghasia katika jimbo la Ituri, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kunaendelea kuwalazimsiha watu kuhama na kuhatarisha maisha yao.

Takwimu za hivi bunde zinaonyesha kuwa takriban raia sita waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa kufuatia mapigano ya silaha katika eneo la Djugu, kulingana na mamlaka ya eneo hilo.

Takwimu zinaonyesha kuwa tangu mwanzoni mwa Mei, mapigano katika jimbo hilo tayari yalikuwa yamewalazimisha zaidi ya watu 12,000 kukimbilia kambi ya wahamiaji ya Rhoe, kilomita 70 kaskazini mwa mji mkuu wa jimbo la Bunia.

Kambi hiyo tayari ilikuwa na idadi ya watu zaidi ya uwezo wake kabla ya wahamiaji hawa wapya, ikipokea karibu watu 45,000 waliokimbia makazi yao, licha ya uwezo wa awali wa watu 40,000.

Wasaidizi wa kibinadamu wanaonya kuhusu hatari kubwa ya magonjwa yanayotokana na maji katika kambi hiyo, kwani zaidi ya asilimia 80 ya mashirika yanayofanya kazi ya maji, usafi wa mazingira na usafi huko yalilazimika kusimamisha shughuli zao kutokana na uhaba wa fedha.

UN inasema mpango wa mahitaji ya kibinadamu na mwitikio wa dola bilioni 2.5 kwa DRC unafadhiliwa kwa asilimia 11 tu kwa dola milioni 282, na hivyo kupunguza kwa kiasi kikubwa uwezo wa mashirika ya misaada kutoa msaada muhimu.

Mpango wa Mahitaji ya Kibinadamu na Mwitikio wa dola bilioni 2.5 kwa DRC unafadhiliwa kwa asilimia 11 tu kwa dola milioni 282, na kupunguza kwa kiasi kubwa uwezo wa mashirika ya misaada kutoa msaada muhimu.


CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us