Mwili wa Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis Baba Mtakatifu Francis utahamishiwa kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro siku ya Jumatano saa tatu asubuhi, kusubiria mazishi yake siku ya Jumamosi.
Kulingana na Vatican, kiongozi wa Makadinali, Giovanni Battista Re, ndiye atakayeongoza mazishi hayo.
Adhimisho la Ekaristi litahitimishwa na Novendiales, yaani siku tisa za maombolezo ya kifo cha Baba na misa kwa ajili ya kupumzisha roho ya Baba Mtakatifu Francis.
Kwa mujibu wa Vatican, mwili wa Papa Francis utapelekwa katika Kanisa kuu la Mtakatifu Petro na baadaye kuhamishiwa kwenye groto ya Mtakatifu Maria Major kwa ajili ya kupumzishwa.
Mapema, siku ya Jumatano, jeneza lenye mwili wa Papa litabebwa kutoka kwenye kanisa la Casa Santa Marta hadi kwenye Basilica ya Mtakatifu Petro.
Kadinali Kevin Farrell, Camerlengo wa Kanisa Takatifu la Roma, ataongoza ibada ya kutafsiri tarehe 23 Aprili, itakayoanza saa tatu asubuhi kwa muda wa maombi.
Maandamano hayo yatapitia maeneo ya Santa Marta Square na Square of the Roman Protomartyrs, kulingana na ofisi ya Papa.
Maandamano hayo yatatoka kupitia Tao la Kengele kwenye Uwanja wa Mtakatifu Petro na kuingia kwenye Kanisa kuu la Vatican kupitia mlango wa kati.
Katika Madhabahu ya Kuungama, Kardinali Camerlengo ataongoza Liturujia ya Neno, na hapo baadaye ziara za kuutembelea mwili wa Papa wa Roma zitaanza.