Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amejitolea kuwa mwenyeji wa mkutano utakaojumuisha viongozi wa Urusi, Ukraine, pamoja na Marekani, kufanya jiji la Istanbul kuwa "kituo cha amani."
Akizungumza baada ya mkutano wa baraza la mawaziri siku ya Jumatatu, Erdogan amesema “matarajio yake makubwa" ni kuwaleta pamoja Rais wa Urusi Vladimir Putin na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy jijini Istanbul au Ankara.
"Ningependa pia kumleta [Rais wa Marekani Donald] Trump,” alisisitiza, huku wajumbe wa Urusi na Ukraine wakikutana jijini Istanbul kwa hatua ya pili ya majadiliano.
Erdogan alitangaza kuwa mkutano wa viongozi kuja pamoja nchini Uturuki, pia “atakutana nao kwenye mkutano huo ili kufanya jiji la Istanbul kuwa kituo cha amani.”
Alipongeza mazungumzo ya Jumatatu kama “hatua muhimu” licha ya matukio ya Jumapili nchini Urusi, yaliyohusisha mashambulizi ya angani usiku ya Ukraine kwa kutumia ndege 162 zisizokuwa na rubani, zikilenga zaidi ya ndege za kijeshi za Urusi 40, ikiwemo A-50, Tu-95, na Tu-22M3 zenye uwezo wa kubeba silaha za nyuklia.
Yanayoendelea nchini Syria
Akizungumzia kuhusu Syria, alisema: “Huku Syria ikiendelea kupata ustawi na amani, tunaamini kuwa majirani zake na nchi zote kwenye kanda hii watafaidika kutokana na hili”.
Erdogan aliridhishwa na uamuzi wa mataifa ya Ulaya kuwaondolewa vikwazo Syria.
Rais wa Uturuki alitangaza,kuwa pamoja na kampuni ya Uturuki ya AJet kufanya safari zake za mara kwa mara za ndege kuelekea Syria, shirika la ndege la Syria Airlines pia litaanza safari zake za ndege hadi Uturuki hivi karibuni.