AFRIKA
4 dk kusoma
Mtazamo wa picha: Kuzingatia maadili katika upigaji picha
Kama maadili hayatatumika katika upigaji picha,huenda kukawa na mkanganyiko,wa kusambaza taswira za ukoloni kutumika katika masuala ya afya,na mashirika ya misaada katika wakati wa sasa.
Mtazamo wa picha: Kuzingatia maadili katika upigaji picha
Picha zina uwezo wa kuonesha mtazamo tofauti wa mtu na namna wengine wanavyokuona. / TRT Afrika English
14 Machi 2025

Mpiga picha kutoka mataifa yaliyoendelea kiuchumi na mwenye vifaa vya kisasa anapewa jukumu la kupiga picha kuhusu matatizo ya afya katika jamii za mataifa ambayo hayajaimarika kiuchumi.

Picha hizi zinatumika na shirika la misaada ya afya duniani na mashirika mengine ya hisani ambayo yanategemea zaidi picha kuonesha milipuko ya magonjwa na migogoro kwa ajili ya kuendeleza kazi za mashirika yao.

Wakati mwingine,picha hizi zinaweza kukosa maadili na kuzidisha hali ya kutokuwa sawa ambayo inahitaji kuangaziwa.

Suala la ukoloni

Mwandishi wa vitabu na mwanachuoni kutoka Kenya Ngugi wa Thiong’o alizungumzia suala la kujivua lugha ya kikoloni. Akielekeza maoni yake kwa waandishi wa masuala ya Afrika, alikabiliana na changamoto ya kutumia lugha kama Kiingereza,Kifaransa,kuliko kutumia lugha zao za asili.

Alisisitiza kutumia lugha za Kiafrika kuna jukumu muhimu katika kuimarisha utamaduni wa taifa, historia na utambulisho.Na kama ilivyo kwa lugha,picha pia zina jukumu muhimu kwa utamaduni wa taifa, historia na utambulisho.

Unapopiga picha unaangazia sehemu muhimu na nini unachotaka kukionesha,simulizi au ujumbe unaolenga kuutoa.

Simulizi,au ujumbe wa picha utakuwa kama ‘balozi’ anayewakilisha mtu au maudhui ya picha.

Kwa hiyo, picha, zina uwezo ambao unaweza kuathiri namna mtazamo wa mtu unavyokuwa na namna watu wanavyomuona.Hili linaweka namna uhusiano wa mtu na dunia ulivyo.

Kama maadili hayatatumika katika upigaji picha,huenda kukawa na mkanganyiko, wa kusambaza taswira za ukoloni kutumika katika masuala ya afya,na mashirika ya misaada katika wakati wa sasa.

Suala la idhini, umuhimu na maadili

Wakati picha inapigwa kuomba ruhusa na kufkiria umuhimu wake ni masuala yanayozingatiwa.

Picha zinazoonesha mtu akiwa katika hali mbaya, na mazingira mabaya ya kiafya zimepigwa na kutolewa kote duniani, kufanya mtu huyo adhalilishwe na kudharauliwa. Picha kama hizi zinazua suala la kama idhini ilipatikana kutoka kwa mtu aliyepigwa picha na uadilifu katika picha yenyewe.

Kuangalia hili kwa makini,kundi la watafiti wa masuala ya afya duniani walichunguza kuhusu heshima na uadilifu unaotumika katika kuweka picha za masuala ya afya duniani.

Utafiti wao ulianzisha vigezo muhimu vya kuzingatiwa:ushahidi wa idhini, umuhimu wa picha hiyo,uadilifu na heshima kwa watu na makundi yaliyopigwa picha.Utaratibu huo bado ni mpya,na bado wadau katika sekta ya afya hawajaanza kuutumia.

Zaidi ya hayo,mashirika kadhaa ya kimataifa yametoa miongozo ya upigaji picha.

Miongozi hii huwa haizingatiwi sana, licha ya kutambuliwa na kutakiakana kuwepo kwa heshima,idhini,uadilifu na usawa.

Kuhakikisha uadilifu na usawa

Pale ambapo mashirika wameweka kanuni za upigaji picha,ni jukumu la mpigaji picha kufwata utaratibu huo.

Hata hivyo,wapiga picha hawana uwezo wa kuangalia namna picha hizo zinavyotumika na kusambazwa.

Kwa hiyo,mashirika yanawajibika kuhakikisha uadilifu ambapo wachapishaji,watu wa mawasiliano na wahariri wanazingatia kanuni hizo.

Mpiga picha anaamia picha gani inafaa itumike na picha gani zinafaa kusambazwa.

Na wao ndiyo wenye jukumu la kuamua picha gani zinafaa zipigwe kwa idhini ya wenyewe na kuhakikisha kuwa wanazingatia heshima yao.

Wakati idhini inapatikana kutoka kwa yule aliyepigwa picha,inatakiwa kuwa na ushahidi wa hilo na mashirika yapate ushahidi huo.

Kwa njia hii,mashirika na wapiga picha wanafanya kazi pamoja kuanzisha msingi wa upigaji picha kwa kuzingatia maadili na kuchapisha.

Wapiga picha wanaozingatia sheria za uadilifu wanatoa picha na maelezo ya muktadha wa picha hii pamoja na kumzungumzia aliyehusishwa kwenye picha hiyo.Kuhakikisha kuwa sauti ya mhusika imeheshimiwa na kuwakilishwa kwa njia sahihi.

Njia nyingine ya kuwasilisha muktadha na sauti za wahusika ni kupata wapiga picha wanaotoka eneo husika.Kupitia kushirikiana na watu wa eneo husika na kuwahusisha wataalamu wa eneo fulani, wenye ufahamu wa masuala yao na mila zao, watapata picha zenye kuonesha muktadha halisi unaotakiwa.

Katika kitabu chake,The Foreign Gaze, Seye Abimbola ameandika,‘… Picha, ina uwezo wa kuonesha muelekeo wa namna tunavyojiandaa na namna tunavyoona au kusema’, kwa hiyo, watu wanaotoka eneo husika wanaweza kuratibu hali na kuhakikisha kuwa tunachiokiona kinaashiria hali halisi ya picha iliyopigwa.

Picha ni chombo muhimu cha kutoa simulizi. Kama ilivyoelezwa,na kwa idhini ya mwandishi wa vitabu wa Kenya na mwanachuoni Ngugi wa Thiong’o, upigaji picha una jukumu muhimu la kuonesha utamaduni, historia na utambulisho wa taifa.

Kutozingatia maadili na upigaji picha usio sahihi unaendeleza simulizi iliyopindishwa na kuathiri utambulisho na heshima ya taifa.

Mwandishi wa makala, Ayan Hag Hersi, ni mwandishi na mtafiti. Amewahi kufanya kazi na shirika la habari la BBC, WHO na SIPRI. Anaandika kuhusu uadilifu na masuala ya afya duniani.

Kanusho: Maoni haya ya mwandishi hayaakisi maoni,msimamo au sera ya uhariri ya TRT Afrika.

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us