Uturuki haitasahau kamwe mshikamano wa watu wa Azerbaijan baada ya matetemeko ya ardhi yaliyokumba kusini mwa Uturuki mnamo Februari 2023, Rais Recep Tayyip Erdogan alisema Alhamisi.
Akizungumza katika hafla muhimu ya kuwakabidhi nyumba kwa walioathiriwa na tetemeko la ardhi katika mkoa wa Kahramanmaras wa Uturuki pamoja na mwenzake wa Azerbaijan Ilham Aliyev, Erdogan alisema kuwa Azerbaijan ni moja ya nchi za kwanza zilizoisaidia nchi yake baada ya tetemeko hilo.
Akisisitiza kwamba Baku (mji mkuu wa Azergaijan) imekuja na kila kitu ilichokuwa nacho kuponya majeraha baada ya tetemeko hilo, pia alielezea kuishukuru Azerbaijan katika kusaidia ujenzi wa nyumba za baada ya tetemeko hilo.
"Bila kujali hali ya ulimwengu na katika eneo letu, kipaumbele chetu kiko wazi," rais wa Uturuki alisema, akiongeza kuwa wana wanatarajia uponyaji wa "haraka iwezekanavyo" kwa majeraha yaliyosababishwa na maafa ya karne.
Aliyev anasifu umoja na udugu
Rais wa Azabajani Ilham Aliyev pia alieleza kuwa watu wa Azerbaijan walichukulia matetemeko ya ardhi yaliyopiga kusini mwa Uturuki mnamo Februari 2023 kama msiba wao, Aliyev alisema "makumi ya maelfu" ya Waazabajani walianza kutekeleza "wajibu wao wa kindugu" kwa kutoa misaada ya kibinadamu.
Aliyev alisisitiza kwamba idadi hiyo hiyo ya watu walipewa nyumba mpya kwa muda mfupi kufuatia matetemeko hayo, uthibitisho wa “ahadi, upendo na azimio kubwa la Erdogan kuelekea watu wake.”
"Wakati huo huo, hii pia ni ushahidi wa Uturuki yenye nguvu, kwa sababu ni serikali yenye nguvu tu inayoweza kufanya kazi kubwa ya ujenzi kwa muda mfupi," Aliyev alisema, na kuongeza kuwa zaidi ya wafanyakazi 1,000 wa Kiazabajani walitumwa mara moja huko wakati huo.
Alisema watu wapatao 53 waliokolewa kutoka kwa vifusi na wafanyakazi wa Azerbaijan, huku watu wengine 3,200 wakipewa msaada wa matibabu na madaktari wa Azerbaijan katika hospitali mbili.
"Azabajani daima imekuwa upande wa Uturuki na pia Uturuki daima imekuwa upande wa Azerbaijan. Leo, ushiriki wangu pamoja na ndugu yangu mpendwa katika ufunguzi wa sehemu za nyumba za 'Azerbaijan' ni ushahidi zaidi wa umoja na urafiki wetu," alisema, akielezea kuanzishwa kwa mtaa wa majumba mapya kama "tukio kubwa."
Amesema udugu na umoja baina ya nchi hizo mbili ni jambo muhimu sio tu kwa eneo hili, bali pia katika kiwango cha kimataifa, akikumbusha kuwa Azimio la Shusha lilipandisha rasmi uhusiano wa Uturuki na Azerbaijan hadi kufikia kiwango cha muungano.
Alitaja uungaji mkono wa Uturuki kwa Azabajani kuhusu suala la Karabakh kutoka siku za kwanza za mzozo wa siku 44 dhidi ya Armenia mnamo 2020, akielezea mshikamano wa Uturuki "ulitupa nguvu zaidi."
"Watu wa Kahramanmaras walionyesha azimio kubwa mbele ya tetemeko la ardhi la kutisha. Hawakuvunjika moyo au kupinda. Walijua na waliamini kwamba nyuma yao kulikuwa na kiongozi mwenye nguvu - Recep Tayyip Erdogan. Nyuma yao inasimama Uturuki yenye nguvu," aliongeza.
Mnamo Februari 6, 2023, matetemeko ya nguvu ya 7.7 na 7.6 yalikumba mikoa 11 ya Uturuki - Adana, Adiyaman, Diyarbakir, Elazig, Hatay, Gaziantep, Kahramanmaras, Kilis, Malatya, Osmaniye na Sanliurfa.
Zaidi ya watu milioni 13.5 Uturuki wameathiriwa na matetemeko hayo, pamoja na wengine wengi kaskazini mwa Syria.
Viongozi hao wawili walihudhiria hafla ya kuzindua nyumba mpya zilizojengwa baada ya tetemeko la ardhi, ambazo zilijengwa na serikali ya Azabajani na Utawala wa Maendeleo ya Makazi wa Jamhuri ya Uturuki (TOKI), katika Kitongoji cha Azerbaijan cha Kahramanmaras.