AFRIKA
1 dk kusoma
DRC yamuwekea kizuizi cha usafiri Waziri wa Sheria
Constant Mutamba amewekewa kizuizi cha kusafiri akituhumiwa kwa makosa ya usimamizi mbaya wa dola milioni 19 za ujenzi wa gereza.
DRC yamuwekea kizuizi cha usafiri Waziri wa Sheria
Waziri wa sheria wa DRC Constant Mutamba ameshitakiwa kwa matumizi mabaya ya fedha /picha: Wizara ya sheria DRC / Public domain
17 Juni 2025

Waziri wa Sheria wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Constant Mutamba amewekewa kizuizi cha kusafiri baada ya Bunge la Kitaifa Jumapili, Juni 15, kuidhinisha dhidi yake madai ya kesi ya ubadhirifu.

Wabunge 322 kati ya 363 walipiga kura ya kuunga mkono kushtakiwa kwa Mutamba, huku 29 wakipiga kura ya hapana na 12 kutopiga kura.

Katika barua ya Jumatatu kwa Kurugenzi Kuu ya Uhamiaji, Mwendesha Mashtaka Mkuu Firmin Mvonde, alisema kizuizi cha usafiri kilitokana na uamuzi wa bunge wa kuondoa kinga ya Mutamba.

"Ninawafahamisha kwamba ... nimeamua kumkataza Mutamba aliyetajwa hapo juu kuondoka katika Jiji la Kinshasa," Mvonde alisema katika barua hiyo iliyochapishwa na vyombo vya habari vya DRC.

Mutamba anashtakiwa kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi wa gereza la Kisangani, mkoani Tshopo.

Anatuhumiwa kwa makosa ya usimamizi mbaya wa dola milioni 19 kwa ujenzi wa gereza.

Afisa huyo wa serikali anatarajiwa kujiuzulu baada ya kura ya bunge kuondoa kinga yake, vyombo vya habari vya ndani viliripoti kunukuu katiba ya Kongo.


CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us