AFRIKA
1 dk kusoma
Kampuni ya TotalEnergies kuanza tena mradi wa gesi Msumbiji mwaka huu
Kampuni ya TotalEnergies inatarajiwa kuanzisha tena mradi wa gesi wa dola bilioni 20 nchini Msumbiji mwaka huu, Afisa Mtendaji Mkuu Patrick Pouyanne alisema siku ya Jumatano.
Kampuni ya TotalEnergies kuanza tena mradi wa gesi Msumbiji mwaka huu
Msumbiji. / Reuters
18 Juni 2025

Kampuni ya nishati ya TotalEnergies imetangaza kujiandaa kuanza tena mradi wa gesi nchini Msumbiji baadaye mwaka huu, Afisa Mtendaji Mkuu wa shirika hilo alithibitisha alipoulizwa kwenye mkutano mjini Tokyo, Japan.

Walilazimika kusitisha mradi huo 2021, kutokana na mashambulizi ya wapiganaji, katika maeneo ya kaskazini mwa nchi. Wafanyakazi waliokuwepo kanda ya Cabo Delgado waliondolewa na shughuli zikasitishwa kutokana na mashambulizi hayo.

“Hali ya usalama imeimarika kwa sasa,” Pouyanne alisema,Sasa ni kwa serikali ya Msumbiji kuhakikisha kuwa inaidhinisha sisi kurejea kwa kuondoa hali ya hatari.”

Utakapokamilika mradi huo utakuwa na uwezo wa kuzalisha tani milioni 13.12 za gesi kwa mwaka.

TotalEnergies ndiyo wanaoongoza katika uwekezaji kwa mradi huo wakiwa na hisa za 26.5%, ikifuatwa na kampuni ya Mitsui & Co ambayo hisa zake ni 20%, huku shirika la serikali la Msumbiji ENH likiwa na hisa 15%. Mashirika ya India na Thailand yanamiliki hisa zilizobakia.

CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us