AFRIKA
2 dk kusoma
Kenya yapokea chanjo za watoto baada ya kukosekana kwa miezi 6
Kulikuwa na wasiwasi mkubwa wa kukosekana kwa chanjo muhimu kote nchini huku vituo vingi vya afya vilipotoa hofu kwani chanjo hizo ni muhimu sana mtoto anapozaliwa.
Kenya yapokea chanjo za watoto baada ya kukosekana kwa miezi 6
Chanjo za kifua kikuu na polio zimesafirishwa kwa vituo tofauti nchini ambapo kulikuwa na ukosefu / Picha: Wizara ya afya Kenya / Public domain
12 Juni 2025

Wizara ya Afya nchini Kenya inawaomba wazazi ambao watoto wao hawakupata chanjo ya BCG ya kukinga kifua kikuu na Polio katika kipindi cha miezi 6 iliyopita, kuwapeleka watoto wao ili kupata chanjo hizo. Hatua hii inakuja baada ya chanjo hizo kukosekana kwa zaidi ya miezi sita. Hata hivyo, kwa mujibu wa serikali, chanjo hizo hivi sasa zimewasili.

Kaunti 12 kati ya 47 ziliripoti kuwa na akiba ya chanjo ilikuwa imekwisha kabisa.

Waziri wa Afya Aden Duale alitangaza kuwa nchi hiyo sasa imepokea dozi milioni 3 za chanjo ya BCG, ambayo hutumiwa sana kuzuia kifua kikuu na dozi milioni 3.2 za chanjo ya polio ya mdomo.

“Peleekeni watoto wenu katika vituo vya afya vilivyopo karibun nanyi ili waate chanjo hii au kama walikosa hapo awali, chanjo sasa inapatikana,,” Waziri Duale alisema.

“Huu ni wakati wa kuhakikisha kila mtoto analindwa dhidi ya magonjwa yote yanayoweza kukingwa,” aliongezea.

Kulikuwa na wasiwasi mkubwa ya kukosekana kwa chanjo muhimu kote nchini huku vituo vingi vya afya vikihofia kukosekana kwa chanjo hiyo.

Waziri Duale anasema kumekuwa na mashauriano kati ya Wizara ya Afya na Hazina ya Kitaifa ili kuhakikisha hakuna usawazisho wa bajeti ya nchi utakaoathiri chanjo.

Kwa hivyo amebainisha kuwa pesa zinazokusudiwa chanjo lazima ziwekewe uzio na zitolewe haraka kwani mitindo mingi ya kimataifa wakati mwingine haikubaliani na kuchelewa kwa malipo.

Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us