Mashambulizi katika jimbo la kaskazini kati mwa Nigeria la Plateau yamesababisha mauaji ya watu wasiopungua 20 wiki hii, serikali za mitaa na vyanzo vya mashirika ya misaada vilisema siku ya Jumatano, katika mapigano yaliyozidi siku za hivi karibuni.
Mashambulizi hayo matatu tofauti kote katika eneo la serikali ya mitaa la Mangu yanafuata msururu wa mashambulizi na kulipiza kisasi ambayo yanaaminika kuanza wakati walipokuwa kwenye migodi, mwenyekiti wa baraza la eneo hilo Emmanuel Bala ameliambia shirika la habari la AFP.
Kwa muda mrefu wafugaji wa jamii ya Fulani wamekuwa wakikabiliana na wakulima katika jimbo la Plateau, wengi wao wakiwa Wakristo, wakigombania ardhi na raslimali.
Mashambulizi katika eneo hilo mara nyingi ni kwa misingi ya kikabila na kidini.
Kulipiza kisasi
"Wakati mmoja wazawa walikuwa kwenye migodi, walishambuliwa" na mapanga, ingawa hakuna aliyeuawa, Bala aliiambia AFP.
Kufuatia msururu wa kulipiza kisasi kwa pande zote mbili, mashambulizi matatu yalifanyika Jumatatu na Jumanne, na kusababisha mauaji ya watu wasiopungua 20, Bala amesema.
Watu wanane waliuawa Jumanne usiku katika kijiji cha Chinchin na walioshukiwa kuwa watu wa jamii ya Fulani, Bala alisema.
Mashambulizi hayo yakafuatwa na mengine siku Jumatatu nje ya mji wa Langai, ambapo watu watano waliuawa.
Ukatili wa kugombania sehemu ya mifugo
Pia siku ya Jumatatu, watu wasiojulikana waliwaua watu saba katika wilaya ya Bwe.
Watu wa jamii ya Fulani katika eneo hilo pia wameshambuliwa katika siku za hivi karibuni kufuatia mashambulizi yaliyolaumiwa kwa watu wa jamii yao, Bala alisema.
Afisa mmoja wa shirika la Msalaba Mwekundu amethibitisha idadi ya waliouawa Chinchin na kusema kuwa idadi ya waliouawa katika kipindi cha saa 24 huenda ikafika 21.
Ardhi inayotumiwa na wakulima na wafugaji katikati mwa Nigeria inakuwa haina rotuba tena kutokana na mabadiliko ya tabianchi na watu kujenga makazi, jambo linalosababisha kugombania sehemu chache.
Kulipiza kisasi kikatili
Unyakuzi wa ardhi, vurugu za kisiasa na kiuchumi baina ya wakazi na wale wanaoonekana kama wakuja kutoka nje, pamoja na wahubiri wa dini wenye misimamo mikali, kumezidisha migawanyiko katika kipindi cha miongo ya hivi karibuni.
Vurugu zinapozidi, kunaweza kumaanisha kulipiza kisasi kwa njia ya ukatili ambayo mara nyingi inafanyika baina ya jamii.
Misururu wa mashambulizi katika jimbo la Plateau na jimbo jirani la Benue imesababisha mauaji ya watu zaidi ya 150 mwezi Aprili pekee.
Huku mauaji ya watu mashuhuri yaliyosababisha wafugaji kulaumiwa nchi nzima, pia wafugaji wenyewe katika kanda hiyo wanasema wao wanashambuliwa kikatili na wakulima, ardhi yao inanyakulia na mifugo kuwekewa sumu.