Na Jolezya Adeyemo
Moja ya alama muhimu katika Makumbusho ya Taifa ya Zambia,mjini Lusaka ni fuvu la mwanamume wa Rhodesia.
Fuvu hili liligunduliwa 1921 katika mji wa Kabwe, safari ya saa tatu kwa gari kutoka Lusaka,limeelezwa kuwa “fuvu la kwanza la mwanadamu kuwahi kugunduliwa barani Afrika.”
Hata hivyo,kuna kitu kimekosekana kwenye maonesho hayo.Kile utakachokiona mjini Lusaka siyo fuvu halisi la mwanamume wa Rhodesia,bali ni mfano wake.
Mwaka 1921,Zambia ilikuwa chini ya utawala wa kikoloni na fuvu lilipogunduliwa,Waingereza walilisafirisha na kulikabidhi kwa pale kunakojulikana sasa kama Makumbusho ya Kihistoria ya Taifa ya London, lipo kwenye maonesho hadi leo.
Wito wa Haki
Mapema 2023,nilitembetelea Makumbusho ya Taifa na muongozaji wangu alinihakikishia kuwa mwanamume wa Rhodesia, maarufu Mwanamume wa Kabwe,atarejeshwa Zambia mwaka huo.
Kwa bahati mbaya,hili bado halijafanyika.Tangu 1972,serikali ya Zambia ilifanya kampeni ya kurejeshwa kwa mwanamume wa Rhodesia,lakini harakati zao hazijafanikiwa mpaka leo.
Shirika la UNESCO lilipitisha makubaliano mwaka 2024 likiagiza Uingereza irejeshe fuvu hilo,bila mafanikio.
Mwanamume wa Rhodesia ni moja kati ya alama za kihistoria na za kitamaduni zilochukuliwa kutoka Zambia na mataifa mengine ya Afrika ambazo sasa ziko katika majumba ya makumbusho barani Ulaya.
Alama hizi za kale siyo tu zilikusanywa;zilichukuliwa bila idhini chini ya utawala wa ukoloni,kutoheshimu umuhimu wao kwa jamii ambazo wamechukuwa kutoka kwao.
Kwa sasa,zimebaki kwenye taasisi ambazo wanafaidika kutokana nazo,ilhali nchi zao za asili zinanyimwa fursa ya kuelimisha watu wao kuhusu asili ya utamaduni wao – pamoja na faida za uchumi zinazotokana nao.
Kuna alama za kale 500,000 ambazo ziko katika taasisi kadhaa kote barani Ulaya (na Marekani).
Katika makumbusho ya Musée royal de l’Afrique Centrale, ambayo pia inajulikana kama Makumbusho ya Afrika,kuna alama 180,000.
Makumbusho haya yana asili yake kutoka enzi za Mfalme wa Ubelgiji Leopold wa pili,ambaye alitawala Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa ukatili kama koloni lake binafsi na inakadiriwa raia wa Congo milioni 10 waliuawa wakati wa utawala wake.
Mwaka 1897, wanaume,wanawake na watoto wa Congo 267, walichukuwa kwa lazima kupelekwa Ubelgiji na kuwekwa kwenye sehemu ya kama ya wanyama ili kujionesha umuhimu wa utawala wa kikoloni.
Maonesho hayo maarufu ndiyo yaliyokuwa Makumbusho ya Afrika, ambayo yako kwenye sehemu hiyo hiyo. Hii ni moja tu kati ya simulizi nyingi mbaya za unyakuzi wa alama za kale za Afrika ambazo ziko katika maeneo mbalimbali Ulaya.
Kuweka kumbukumbu ya kidijitali
Katika miaka ya hivi karibuni,kurejesha alama hizo kwa njia za kidijitali imekuwa njia moja ya kufanya Waafrika wahisi wanamiliki alama hizi.
Kwa mfano,Makumbusho ya Historia ya Wanawake ya Zambia imeanza kuhifadhi alama za kale ambazo ziko Sweden. Makumbusho ya Sweden,yana alama za kale 600 kutoka Zambia.
Makumbusho hayo yameanza kurejesha alama hizo kidijitali kwa lengo la kuwapa elimu watu wa Zambia kuhusu utamaduni, kwa umuhimu wa alama hizi kwa jamii,ambazo zilichukuliwa kutoka ardhi ya Zambia miaka mingi iliyopita.
Miongoni mwao ni matenga ya uvuvi na vinyago vya sherehe,miongoni mwa zingine.Wakati hatua hii ikielezwa kuwa ni muhimu,hatua zaidi zinahitajika.
Mfumo wa kidijitali unasaidia sana lakini hauwezi kuchukuwa nafasi ya alama zenyewe halisi,na haziwezi kurekebisha uwizi na ukandamizaji wa kihistoria.
Wengine wanasema kuwa alama hizi ni za watu wote,siyo tu kwa nchi zao za asili.
Hata hivyo, lakini hii haitumiki kwa alama za kale kutoka Ulaya; hakuna mtu aliyesema alama za kale za Ugiriki au mafuvu yalogunduliwa Ulaya yapelekwe kwenye makumbusho ya Afrika kufaidisha "watu."
Baadhi ya mataifa ya Ulaya yameanza kuchukua hatua za kurejesha baadhi ya alama hizo.Kwa mfano,Ufaransa,imerejesha alama za kale 26 Benin in 2021,kuonesha hatua muhimu katika kukiri makosa ya zamani.
Hata hivyo,kuna alama nyingi za utamaduni wa watu wa Benin bado ziko Ufaransa.Pia,kuna matukio mengine ya kukataa kurejesha"kwa muda"alama zilizoibiwa kwenye nchi zao za asili,ambayo ni ya kushangaza na kukosa heshima kwa kuwa mtu hawezi kumpa mwingine kitu kwa muda ambacho kwanza hakikuwa chako.
Msimamo mmoja kuhusu kurejeshwa kwa alama za kale
Umoja wa Afrika umekuwa ukipigania kurejeshwa kwa alama za kale zilizoibwa barani Afrika,ikiwemo kupitia ushirikiano wa 2023 na Jumuiya ya Caribbean (CARICOM) ambayo ilitaka kulipwa fidia na kurejeshwa kwa alama za kale za kitamaduni.
Baraza lake la Uchumi,Jamii,na Utamaduni (ECOSOCC) pia limesisitiza kuwa kulipwa fidia ni sehemu muhimu ya kushughulikia ukandamizaji wa haki wa kihistoria. Msimamo wa pamoja unsaidia juhudi hizi—kwa kufanya kazi pamoja, mataifa ya Afrika yanaweza kuweka shinikizo kubwa la kidiplomasia na kisheria kuliko eneo lingine lolote.
Lakini pia kurejeshwa kwa alama za kale za kitamaduni na kihistoria zinahitaji miundombinu ya uhakika ili kuweka alama hizo. Kurejeshwa kwa alama hizi lazima kupangwe vizuri.
Kurejeshwa kwa alama za kale siyo tu kuzirejesha; ni kurejesha utambulisho, heshima, na historia. Kurejeshwa kwa mali za kitamaduni za Afrika ni jambo lilitakiwa kufanyika zamani, na ni wakati sasa kwa taasisi za Magharibi kukubali kuwa alama za kale zilizoibwa haziwezo kubaki katika mataifa ya kigeni milele.
Mwandishi, Jolezya Adeyemo,ni mwandishi wa kujitegemea mjini Lusaka,mshauri wa uhariri, na mratibu wa mikakati. Anashughulika na Historia ya Afrika na utamaduni wake. Ana shahada ya ushirikiano wa kimataifa kutoka Chuo Kikuu cha Queensland nchini Australia.
Kanusho: Maoni haya ya mwandishi hayaakisi maoni,mitazamo na sera ya uhariri ya TRT Afrika.