AFRIKA
1 dk kusoma
Waziri wa Msumbiji aeleza matumaini ya mradi wa gesi
Mpango wa TotalEnergies kuanzisha tena mradi wa uchimbaji gesi ni jambo la kuleta matumaini, amesema waziri wa nishati wa Msumbiji Estevao Pale.
Waziri wa Msumbiji aeleza matumaini ya mradi wa gesi
Msumbiji. / Reuters
20 Juni 2025

Waziri wa nishati wa Msumbiji alisema siku ya Ijumaa kuwa serikali haijapokea ombi rasmi kutoka kwa kampuni ya TotalEnergies kuhusu kuanzisha tena mradi wa gesi wa dola bilioni 20 nchini humo. Hata hivyo, alieleza matumaini yake kuwa mipango ya TotalEnergies' kuanzisha mradi huo kuwa hatua nzuri.

Baada ya mkutano na waziri wa viwanda wa Japan, Muto Yoji, waziri wa nishati wa Msumbiji Estevao Pale, aliwaambia waandishi wa habari kuwa hali ya dharura iliyokuwepo itaondolewa pale utaratibu wa kuhakikisha usalama wa mradi kuanza tena utakapokamilika.

Pale alieleza kuwa serikali inafanya kila iwezalo kuona kuwa mradi huo unaanza tena.

Alisema wanafanya kazi pamoja na washirika wake kuimarisha usalama wa kuanzishwa tena kwa mradi huo.

Siku ya Jumatano Afisa Mkuu Mtendaji wa TotalEnergies, Patrick Pouyanne, alisema katika mkutano wa nishati jijini Tokyo, Japan kuwa mradi unatarajiwa kuanza tena baadaye mwaka huu.

CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us