MICHEZO
1 dk kusoma
Mwamuzi wa EPL Coote aliyefutwa kazi ashtakiwa kwa video ya kumkashifu Klopp
Aliyekuwa mwamuzi wa Ligi Kuu ya England David Coote ameshtakiwa na Shirikisho la soka nchini humo kwa matamshi aliyoyatoa kwa kocha wa zamani wa Liverpool Jurgen Klopp katika video ambayo ilisambazwa katika mitandao ya kijamii.
Mwamuzi wa EPL Coote aliyefutwa kazi ashtakiwa kwa video ya kumkashifu Klopp
Mwamuzi David Coote. / Reuters
18 Juni 2025

Mwamuzi huyo mwenye umri wa 42 alisimamishwa na Shirikisho hilo mwezi Novemba 2024 baada ya video kumuonesha akitoa matamshi ya kejeli kuhusu kocha huyo raia wa Ujerumani na timu ya Liverpool.

Coote alifutwa kazi mwezi mmoja baadaye kufuatia "uchunguzi wa kina" kuhusu mienendo yake.

Shirikisho la Soka limemshtaki Coote kukiuka sheria ya bodi hiyo, ya kuwa na mienendo yasiyo na nidhamu na kutumia lugha ya matusi.

Shirikisho linasema alizungumzia kuhusu uraia wa Klopp katika video hiyo ambayo linasema ulikuwa "ukiukwaji mkubwa" wa maadili.

Hata hivyo, Coote aliondolewa madai ya kujihusisha na kamari wakati mwamuzi huyo alipozungumzia kumuonesha kadi ya njano mchezaji mmoja kabla ya mechi kuanza.

CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us