Mambo matano muhimu kuhusu Kapteni Ibrahim Traore wa Burkina Faso
Mambo matano muhimu kuhusu Kapteni Ibrahim Traore wa Burkina Faso
Kiongozi wa nchi mwenye umri mdogo zaidi duniani, Ibrahim Traore, mwenye umri wa miaka 37, anshuhudia umaarufu wake ukiongezeka hasa miongoni mwa vijana tangu kuchukua mamlaka katika mapinduzi ya kijeshi Septemba 2022.
22 Mei 2025

Rais wa Mpito wa Burkina Faso Kapteni Ibrahim Traore ni kiongozi anayevutia watu wengi barani Afrika na kwengineko. Anapendwa sana na vijana wanaomuona kama kiongozi wa wa kuleta mapinduzi.

Haya hapa ni mambo matano muhimu kuhusu kiongozi huyo:

Rais mwenye umri mdogo zaidi

Kapteni Ibrahim Traore ndiye rais wa nchi mwenye umri mdogo zaidi duniani, aliyezaliwa Machi 14, 1988. Ni mdogo hata kuliko Rais wa Ecuador Daniel Noboa, rais wa pili mwenye umri mdogo zaidi duniani, kwa takriban miezi mitatu na nusu, na umri wa miaka 55 kuliko Rais wa Cameroon Paul Biya, rais wa nchi mwenye umri wa miaka 92.

Safari yake ya kijeshi

Traore alijiunga na jeshi la Burkina Faso mwaka wa 2009 na kupanda ngazi hadi kuwa kapteni mwaka wa 2020. Alikuwa sehemu ya kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kulinda amani nchini Mali na baadaye alipigana dhidi ya waasi nchini mwake, na hivyo kupata sifa. Kiongozi huyo alichukua mamlaka kupitia mapinduzi ya kijeshi mnamo Septemba 2022, na kumpindua Kanali Paul-Henri Damiba.

Muungano wa Sahel

Safari ya kwanza ya nje ya Traore kama mkuu wa nchi ilikuwa Mali, ambako alikutana na kiongozi wa kijeshi Kanali Assimi Goita mnamo Novemba 2, 2022. Mali na Niger sasa ni washirika wa karibu wa Burkina Faso na watatu hao tangu wakati huo wameunda kambi inayojulikana kama Muungano wa Mataifa ya Sahel, AES, baada ya kujitenga na ECOWAS.

Safari zake za nje

Nchi pekee ya Kiafrika ambayo Traore ametembelea nje ya AES ni Ghana, ambapo alihudhuria kuapishwa kwa Rais John Mahama mnamo Januari 7, 2025. Nje ya Afrika ametembelea nchi ya Urusi.

Maisha ya kibinafsi

Wakati wakuu wengi wa nchi mara nyingi huonekana na wenzi wao na watoto hadharani, kwa Traore mwenye umri wa miaka 37, suala la mke au watoto linabaki kuwa la faragha.

Salamu za kipekee

Traore anajulikana kwa salamu zake za ajabu za kupeana tano au kukunja ngumi - kusalimiana na mikono ni nadra sana, zaidi ya hayo yeye ni shabiki mkubwa na mchezaji wa mpira wa miguu.

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us