Kwa karne nyingi, simulizi ya bara la Afrika imejengwa na watu wa nje, historia yake ikiwa ukoloni, utajiri wake kuwa umasikini na hata watu wake kuwa wahangaikaji.
Hata hivyo, nyuma ya ukweli huu, bara la Afrika linafahamika kwa utajiri wake, huko himaya nyingi zikiwa vyanzo vya elimu na maarifa.
Changamoto ya leo si kumbukumbu ya simulizi hizi, lakini namna ya kuunganika na simulizi hizo.
Afrika ina uwezo wa kuondoka simulizi hizo mbaya na kujijengea heshima yenye kustahili.
Asili ya yote
Ngoja tuanze na ukweli usiosemwa: Afrika ndiye mwanzilishi wa vyote, chukulia mifano ya himaya za Aksum, ambazo zilikuwa sehemu ya Ethiopia na Eritrea.
Jamii ya watu wa Aksum, walianza kuchonga mawe makubwa, ilipofika karne ya 4 tu.
Sarafu zao zenye picha za wafalme, zilianza kutumika kwenye dola mbalimbali, ikiwemo Roma.
Pia, kulikuwa na himaya ya Mali. Wakati wa safari yake ya kuelekea Maka mwaka 1324, msafara wa Mansa Musa haukubeba dhahabu tu; bali fahari na uthubutu.
Hata hivyo, utajiri wa Mali ulipatikana zaidi Timbuktu, eneo ambalo wasomi wa nyakati hizi waliandika nyaraka nyingi za sheria, mambo ya anga na utabibu.
Nyaraka ya karne ya 15, iliyoandaliwa Timbuktu, iliwataka madaktari kuhisi pumzi za wagonjwa wao, na sio kutegemea ulozi.
Kuibiwa kumbukumbu
Ukoloni haukuondoka na rasilimali za Afrika tu, bali pia kumbukumbu.
Babu yangu aliwahi kunihadithia kuwa shule za Waingereza ziliwafundisha kuwa historia ilianza mwaka 1471, “baada ya kuwasili kwa wareno.”
Hawakuwa kumtaja Malkia Amanirenas (60 – 10 Kabla ya Kristo), shujaa mwanamke kutoka himaya ya Wakushi aliyewaongoza watu wake dhidi ya uvamizi wa Kirumi.
Makovu yasiyofutika
Nikiwa Kampala mwaka jana, nilikutana na kijana mmoja mwenye umri wa miaka 19, mtaalamu wa kutengeneza program, ambaye alikiri kutowahi kusikia kuhusu mbinu kale za uvunaji maji katika jamii ya Kimaasai.
“Badala yake, walitufundisha kuhusu mambo ya Warumi,” alisema.
Lazima ujiulize mara mbili pindi unapoambiwa kuwa mababu zako walikuwa ni watu wasiostaarabika.
Kabla ya ujio wa watu wa Ulaya, himaya ya Benin (leo ikiitwa Nigeria) ilifanya ujenzi mkubwa wa ardhini wenye urfeu wa kilomita 16,000, kupita ukuta mrefu wa China.
Hadi leo, wahandisi mbalimbali wa Kingeria kama vile Olajumoke Adenowo wanaguswa na ubinifu huo wa kale.
Kuna miji iliyoendelezwa kutokana na biashara, kama vile Mogadishu nchini Somalia, Kilwa (Tanzania) na Gedi (Kenya).
Kufikia karne ya 13, kasri la Husuni Kubwa huko Kilwa lilikuwa na vyoo vya kuvuta.
Wafalme wa Kikushi waliotawala Misri, walijenga Mapiramidi mengi zaidi kuliko jirani zao.
Mfalme Amanirenas alishinda majeshi ya Kirumi na kuingia nao mkataba.
Dondoo
Jamii ya watu wa Nok ilichonga vinyago vilivyoonesha madaraja kwenye jamii, mitindo ya nywele na mbinu za kitabibu.
Sanaa yao, baadaye iliwakosha Wayoruba na Waigbo.
Leo hii, wasanii wa mitaa ya Lagos kama vile Laolu Senbanjo, wamehuisha vinyago hivyo kama mapambano dhidi ya ufisadi.
Kati ya mwaka 1701 hadi 1957, jamii ya watu wa Asante wa Ghana waliendesha serikali yao kwa kutumia katiba ambapo raia walikuwa na uwezo wa kuwaondoa viongozi mafisadi.
Vazi la Kente lilijulikana kama ishara ya umoja barani Afrika.
Tunarudishwa nyuma mpaka kwenye majangwa ya Libya, wakati ambapo Wagaramante walijenga mahandaki ya kupitisha maji kati ya mwaka 500 hadi 700.
Mashimo hayo yenye urefu wa kilomita 50, yaligeuza eneo la Sahara kuwa chanzo kikubwa cha chakula.
Urithi uliounganika
Himaya za Kiafrika hazikuachwa zenyewe.
Msafara wa Wabantu (3000-500), ukianzia Cameroon, ulitandaa na kutengeneza lugha mbalimbali katika mataifa 20.
Kufikia leo, watu milioni 350 barani Afrika wanazungumza lugha za kibantu.
Jijini Johannesburg, nesi Mxhosa na mhandisi kutoka kabila la Wakikuyu wanaweza kujadili siasa, bila kutambua kuwa babu zao walikuwa wamoja.
Kupitia misafara ya Mfecane, himaya ya wazulu iliitengeneza Afrika Kusini, hasa jamii za Sotho, Ndebele na Swazi.
Katika jimbo la Bahia nchini Brazil, visasili vya Kiyoruba kutoka himaya ya Oyo wanaendelea kupamba malkia zao.
Waongoza matambiko wa Haiti, hutumia nguvu kutoka mashujaa wa himaya ya Dahomey.
Nchini Suriname, watu kutoka jamii ya Ndyuka bado wanatumia majina ya Akan, kama vile Kwasi( Jumapili) na Afia (Ijumaa).
Huu ni ushahidi tosha kuwa himaya za Kiafrika hazikudondoshwa, bali zinazidi kutamalaki.
Edna Adan Ismail altumia mifano ya wakunga wa enzi za Sultani Adal.
Kusema ukweli
Wanawake hawa hawaoneshi heshima kwenye historia peke yake, bali wanasema ukweli: Nchi 54 za Kiafrika zimetoka ni matawi ya mti mmoja.
Himaya ya Kongo (1390-1914) ilisambaa Angola, Congo na Gabon. Leo hii, nchi hizo zinachangia lugha ya Kikongo na mifumo ya kitawala.
Mfano mwingine ni Masi Mamombe, mwanaharakati wa Zimbabwe anayetumia nukuu za Nehanda Nyakasikana—kiongozi wa kiroho aliyenyongwa na wakoloni wakati wa maandamano ya mwaka 1898.
“Nehanda hakufa ili tuombe demokrasia,” alinieleza.“Alipoteza uhai wake ili tukumbuke nguvu yetu.”
‘Kumbukeni nguvu yetu’
Nawaacha na kitu ambacho sipaswi kusahau.
Katika maeneo duni ya jiji la Nairobi, vijana kadhaa wanaonesha filamu yenye kuhusu wapigania uhuru wa Mau Mau.
Baadaye wakaanza kuulizana, “Ingekuwa vipi Wangu wa Makeri angekuwa mtawala wa Kikuyu mwaka 1900?”
Kwa muda mrefu sasa, simulizi za Afrika zimekuwa zikiandikwa na wale waliochezea utajiri wake.
Ni wakati muafaka sasa, Waafrika wachukue jukumu la kueleza historia ya bara la Afrika.
Hii inamaanisha kukataa kasumba kuwa Afrika inaakisi mateso, badala yake kusema kuwa bara hili limejaa wabunifu.
Hili litafanyikaje? Elimu ni kila kitu. Ni vyema taasisi za elimu zihusishe mifumo ya elimu za jadi.
Wafanyabiashara waweke kwenye vipaji vya ndani ili kutatua changamoto za Afrika.
Viongozi wa Afrika wanapaswa kutambua kuwa utawala wa kweli sio wa kisiasa tu, ni wa kiutamaduni, kiakili na kiuchumi.
Hili litawezekana tu iwapo tutaacha utegemezi, na tukaamua kujitegemea.
Dunia iko macho wazi, lakini la muhimu zaidi ni kuwa Waafrika wameamka.
Wakati umefikia kwa Afrika kuweka wazi himaya na simulizi zake zilizofichika na tutembee kifua mbele.