UTURUKI
1 dk kusoma
Klabu ya Alves Kablo ya nchini Uturuki yashinda Ligi ya Mabingwa kwa upande wa walemavu
Timu ya walemavu ya Alves Kablo imetwaa ubingwa huo baada ya kuibugiza Wisla Krakow ya Poland kwa jumla ya mabao 6-1, katika mchezo wa fainali uliofanyika jijini Ankara.
Klabu ya Alves Kablo ya nchini Uturuki yashinda Ligi ya Mabingwa kwa upande wa walemavu
Michuano hiyo huandaliwa na Shirikisho la Soka la Walemavu barani Ulaya (EAFF), likihusisha timu za walemavu kutoka Ulaya./Picha: AA
2 Juni 2025

Klabu ya Alves Kablo ya nchini Uturuki imetwaa Ligi ya Mabingwa kwa upande wa walemavu kwa mwaka 2025, baada ya kuifunga Wisla Krakow ya nchini Poland kwa mabao 6-1, katika mchezo wa fainali uliofanyika siku ya Jumapili.

Hadi mapumziko, Alves Kablo walikuwa wakiongoza kwa mabao 4-0, dhidi ya mabingwa hao wa mwaka 2024.

Magoli ya Alves Kablo yalifungwa na David Mendes, katika dakika ya pili na 18, huku Omer Guleryuz akiongeza mawili katika dakika ya 8 na ya 28, Mohcine Chrharh akitupia bao la tano katika dakika ya tisa, na Alican Kuruyamac akipigilia msumari wa mwisho katika dakika ya 50 ya mchezo.

Bao pekee la Wisla Krakow, lilifungwa na Kamil Grygiel katika dakika ya 39.

Michuano hiyo huandaliwa na Shirikisho la Soka la Walemavu barani Ulaya (EAFF), likihusisha timu za walemavu kutoka Ulaya.

Yakifanyika kutoka Mei 30 hadi Juni 1, mashindano ya mwaka huu yalihusisha mataifa mbalimbali, yakiwemo Poland, Italia, Ujerumani, Georgia, Ireland, Hispania na Ufaransa, huku Alves Kablo wakiwa ni wenyeji.

 

CHANZO:AA
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us