AFRIKA
5 dk kusoma
Namna ujasiri wa ukimya ulivyokosekana katika usalama ulimwenguni
Siku hizi kawaida ujasiri hauhitaji kupiga kelele. Unakuwa kimya kimya katika mikutano ya faragha. Inaonesha ari ya kutaka kusikiliza na kuzungumza ndani ya vyumba vya mikutano sehemu ambayo kuna wasiwasi mkubwa.
Namna ujasiri wa ukimya ulivyokosekana katika usalama ulimwenguni
Ujasiri wa kuwa jasiri huenda ikawa ni suala ambalo haliangaziwi sana katika dunia ambayo imesambaratika. / Reuters
3 Juni 2025

Nimewahi kukaa katika ukumbi wa mkutano uliokuwa umejaa watu wengi wakiwa wamevaa suti na sare za jeshi.

Safu ya mbele ikiwa na viti vyeupe viloandaliwa kwa ajili ya waheshimiwa. Nyuma yake walikuwa wanadiplomasia, wapanga mikakati, na wataalamu wa masuala ya usalama.

Vijana waliojitolea wakitembea huku na kule, wakiwa na kamera, wakikaribisha wageni, na kuhakikisha kuwa ratiba inaendelea bila wasiwasi wowote.

Hali ilikuwa ya kuonesha umuhimu lakini kulikuwa kumetulia. Mazungumzo yaliangazia ushindani wa maeneo mbalimbali, vitisho, na uthabiti wa mifumo ya ulimwengu.

Pamoja na majadiliano yote rasmi, fikra zangu zilikuwa kwenye jambo ambalo ni la kawaida sana - ujasiri.

Siyo ujasiri ambao unapatikana kwenye uwanja wa vita au kwenye majukwaa. Ujasiri wa kimya kimya, unaoendelea. Ujasiri wa kuzugumza ukweli wakati maneno yanaweza kuchukuliwa nje ya muktadha.

Ujasiri wa kuwepo sehemu na kusikiliza mazungumzo ambapo uaminifu ni mdogo. Ujasiri wa kuunganisha, na kuwepo wakati kila inapoonekana kuwa kila hatua inaangaziwa.

Ujasiri huu wa kimya kimya ni moja kati ya mambo ambayo hayaangaziwi sana na ambayo ni muhimu katika dunia inayozidi kusambaratika.

Ujasiri chini ya shinikizo

Dunia inabadilika. Kulingana na ripoti ya usalama ya Munich 2025, uwezo haupo tu kwenye sehemu moja.

Badala yake, washiriki wengi wa kikanda na kimataifa sasa hivi wanakuwa sehemu ya mfumo wa kimataifa. Mfumo unamaanisha washirika wengi zaidi na hali ya kutoeleweka. Ushirikiano wa zamani hauko thabiti sana. Uaminifu uko tete.

Mikakati ambayo zamani ilionekana kuwa imara sasa ipo zaidi kimasharti.

Mabadiliko haya siyo tu kisiasa. Yanaathiri namna watu wanavyoamiliana.

Ujasiri wa sasa hivi hauhitaji kelele. Upo kimya kimya katika mikutano ya faragha.

Afrika inaonesha mfano wa namna ujasiri wa kimya kimya unavyoweza kutoa muelekeo wa mazungumzo kuhusu usalama.

Katika makongamano kama ya kimataifa ya usalama kuhusu Afrika (ISCA) na mengine kuhusu usalama, viongozi wa kanda, wataalamu, na mashirika ya kiraia wanakutana kujadili changamoto. Wanazungumza wazi kuhusu ugaidi,kutokuwepo kwa utawala bora, na vizingiti vya maendeleo. Hakuna kuremba.

Katika kongamano la kwanza la ISCA mjini Kigali, Rais wa Rwanda Paul Kagame alizungumza wazi kuhusu umuhimu wa mataifa ya Afrika kuchukua jukumu kamili la amani na usalama wao.

Alisema usalama wa kikweli hauwezi kutoka nje. Ujumbe wake ulikuwa wazi: mabadiliko yanaanza na ujasiri wa kuamini chombo chako mwenyewe na kuongoza, hata kama njia haiko wazi.

TMkutano wa 2023 wa Jukwaa la Tana ulisisitiza kuhusu uthabiti siyo tu uwezo wa kijeshi au ushirikiano na mataifa ya nje. Ni kuhusu kuaminiana na majadiliano ya wazi.

Jukumu la Uturuki katika mazingira ya kidiplomasia linaashiria mchakato kama huo. Kama nchi yenye uwezo kikanda, Uturuki imekuwa na jukumu muhimu la kusaidia kuwepo kwa majadiliano katika maeneo mbalimbali.

Jukumu lake la kusuluhisha matatizo ya nafaka katika Bahari Nyeusi, mazungumzo ya amani kati ya Urusi na Ukraine na kuwa wazi kwa wote washirika wa NATO na mataifa yasiyokuwa ya Magharibi inaonesha dhamira ya Uturuki ya diplomasia ya ujasiri.

Uturuki kuendeleza msimamo wake katika suala la Syria, kuweka sawa masuala ya usalama pamoja na kushiriki michakatao ya kisiasa kama mazungumzo ya Astana, kunaonesha utayari wake zaidi kuendelea kuwepo katika mazingira magumu, hasa katika mazingira ambayo yanahitaji ujasiri.

Kuendelea kuwepo kwake katika majadiliano kunaonesha mkakati mpana: ule ambao unahitaji mazungumzo zaidi kuliko kukaa kando, hata wakati watu wanaposhindwa kukubaliana.

Kwa hali hii, mtazamo wa Uturuki ni mfano wa ujasiri unaotumika kama mkakati.

Kusambaratika na uwezo wa kuaminiana kwa ukimya

Dunia nzima pia inakuwa na tatizo la ushirikiano. Kile ambacho wataalamu wanakiita “kudumaa kwa ushirikiano” kumaanisha kupungua kwa ushirikiani duniani ambapo zamani ushirikiano huo ulikuwepo.

Ripoti kuhusu hatari duniani ya Jukwaa la Uchumi 2025 inaeleza hatari ya kusambaratika. Inazungumzia mgawanyiko, taarifa potofu, na migogoro katika jamii kama inayotishia usalama ulimwenguni.

Haya siyo tu mabadilik ya kimfumo. Yanazingatia misingi ya kibinadamu. Kukataa kuzungumza, kusikiliza, au kushirikiana kunasababisha kuwepo kwa hofu na kurubuniwa.

Katika muktadha huu, ujasiri, unakuwa muhimu sana. Ni wananchi ambao wanashiriki katika mazungumzo haya. Wao ndiyo wanahusika zaidi na majukwaa ya kujenga mifumo ya uwazi. Mwanadiplomasia ambaye anachagua fikra tulivu kuliko kuleta uchochezi.

Hatua hizi zinaweza kuonekana ndogo. Lakini ukiziangalia vizuri, zinajenga msingi wa usalama na kuaminiana.

Mkakati enzi za ugumu

Leo hii suala la usalama haliwezi kufanywa kwa nguvu tu. Linategema uwezo wa taasisi na uhusiano wa kufanya taasisi hizo ziweze kuhimili.

Uthabiti wa mkakati ikiwemo miundombinu, mifumo ya kidijitali, na utayari wa kiuchumi. Lakini pia inajumuisha watu. Watu ambao wako tayari kujitokeza kwa dhati. Watu ambao wanaweza kupambana na kutoaminiana na kuwa na uadilifu.

Ujasiri siyo tu jambo la heshima. Ni raslimali. Unasaidia majadiliano wakati siasa zinapokuwa na mvutano. Unasaidia ushirikiano wakati watu wanapokuwa hawaelewani.

Unajenga ujamii katika jamii zilizofarikiana. Ndiyo unaosaidia wanadiplomasia kurudi katika meza ya majadiliano, wananchi kuzingatia misingi ya kidemokrasia, na taasisi kurekebisha pale mambo panakwenda kombo.

Ujasiri unatakiwa kuwepo katika kila ngazi ya jamii. Siyo tu katika ukumbi wa mikutano au majengo ya serikali. Lazima uwepo katika majadiliano ya kijamii, agenda za vyombo vya habari, taasisi za mafunzo, na mitandao ya kijamii.

Wakati unapojiona kuwa unashindwa kuongea au kuchukua hatua, ukihofia itatafsiriwa tofauti au watu kuhukumu kivingine, fahamu hili: ujasiri wako ni muhimu.

Uamuzi wako wa kuongea ukweli, kusikiliza kwa makini, na bado kuwa msikivu katika ulimwengu wenye kelele nyingi siyo jambo dogo. Ni msingi mzuri. Ndiyo nguvu ya ukimya ambayo ni nguzo ya mifumo iliyosambaratika.

Katika ulimwengu wa leo usioeleweka, kuwa na msimamo thabiti, hata katika mazingira yasiyo rasmi, inaweza kuwa ishara yenye nguvu ya uongozi.

Ujasiri kama huu hauhitaji kutangazwa na vyombo vya habari. Lakini unaweza kuwa ndiyo umekosekana katika kuimarisha usalama duniani.

Mwandishi, Fauziya Ali, ni Rais wa Kimataifa wa Wanawake katika masuala ya Usalama wa Upembe wa Afrika (WIIS-HoA). Ni mtaalamu wa masuala ya Usalama wa watu, Jinsia na AI.

Kanusho: Maoni ya mwandishi hayaakisi maoni, mitazamo na sera za uhariri za TRT Afrika.

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us