Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji nchini Tanzania (EWURA), imetangaza punguzo la bei ya mafuta ya petrol, itakayoanza rasmi Julai 1, 2025.
Katika taarifa yake, EWURA imesema kuwa punguzo hilo linaendana na na utekelezaji wa Sheria Mpya ya Fedha iliyoanza kutumika siku ya Julai 1.
Kulingana na EWURA, watumiaji wa nishati ya petroli jijini Dar es Salaam, watalipia Dola 1.10 (Shilingi za Kitanzania 2,877) kwa lita, kutoka dola 1.11(Shilingi za Kitanzania 2,882) kwa mwezi wa Juni.
EWURA imesisitiza kuwa mabadiliko hayo ya bei yametokana na mabadiliko ya bei ya mafuta katika soko la dunia.
Mamlaka hiyo imesisitiza kuwa bei za bidhaa za mafuta ya petroli zitaendelea kupangwa na soko, kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2015, kifungu namba 166.