AFRIKA
1 dk kusoma
Rais wa Ukraine kukatisha ziara yake ya Afrika Kusini
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amesema amelazimika kukatisha sehemu ya ratiba yake nchini Afrika Kusini baada ya shambulizi la Urusi katika mji mkuu wa Kyiv.
Rais wa Ukraine kukatisha ziara yake ya Afrika Kusini
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amemkaribisha Rais wa Ukraine Zelenskyy / AP
24 Aprili 2025

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy atakatisha ziara yake nchini Afrika Kusini baada ya mashambulizi ya Urusi katika mji mkuu wa Kyiv kuwaua takriban watu tisa.

Rais Zelenskyy aliwasili Afrika Kusini Alhamisi asubuhi kwa mazungumzo na Rais Cyril Ramaphosa wa nchi hiyo kuhusu ushirikiano wa pande mbili na juhudi za kumaliza vita vya Urusi nchini Ukraine.

“Ninakatisha sehemu ya ratiba ya ziara hii na nitarejea Ukraine mara tu baada ya mkutano na Rais wa Afrika Kusini,” alisema katika mtandao wa jamii.

“Leo, nitamueleza Rais Ramaphosa wa Afrika Kusini, ambaye kwa sasa anashikilia Urais wa G20, kuhusu hali na haja yetu ya kuimarisha juhudi za kidiplomasia duniani. Mashambulizi lazima yakomeshwe mara moja na bila masharti,” aliongezea.

TRT Global - Takriban watu tisa wauawa, 63 wajeruhiwa Kiev katika shambulizi la Urusi

Msaidizi mwandamizi wa Rais wa Ukraine amesema mashambulizi hayo kwa raia sharti yasitishwe.

🔗

“Pia tunategemea uungwaji mkono katika masuala ya kibinadamu - katika kuwarudisha wafungwa wetu na watoto wa Kiukreni waliotekwa nyara na Urusi,” Rais Zelenskyy aliongezea.

Rais Zelenskyy amesema shughuli za uokoaji zinaendelea, na vifusi vya majengo ya makazi vinaondolewa. Kufikia Alhamisi asubuhi amesema zaidi ya watu 80 wamejeruhiwa kote Ukraine huku 9 wakiuawa.

Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us