Hawa ndio marais na viongozi wa Afrika waliozikwa nje ya nchi zao
Hawa ndio marais na viongozi wa Afrika waliozikwa nje ya nchi zao
Mahakama ya Afrika Kusini imeweka pingamizi kwenye mazishi ya rais wa zamani wa Zambia, Edgar Lungu huku ikipanga kusikiliza tena kesi hiyo Agosti 4, mwaka huu.
1 Julai 2025

Utata mkubwa umeghubika taifa la Zambia, kuhusiana na mipango ya mazishi ya aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo, Edgar lungu.

Wakati Serikali inataka mwili wa rais huyo wa zamani aliyefariki dunia Juni 5, 2025, urudishwe nyumbani kwa ajili ya kuzikwa, familia yake imesisitiza haja ya kiongozi huyo azikwe nchini Afrika Kusini, ambako alikuwa anapokea matibabu, kwa madai kuwa alikuwa na uhasama na Rais wa Zambia Hakainde Hichilema. 

Hata hivyo, Mahakama ya Afrika Kusini imesimamisha mazishi ya kiongozi, huku ikipanga kusikiliza kesi hiyo Agosti 4, 2025. 

Ikitokea kuwa mahakama ya Afrika Kusini ikaungana na familia ya Lungu, basi huyo hatokuwa kiongozi wa kwanza kuzikwa nje ya nchi yake.

Unamkumbuka Idi Amin Dada wa Uganda?

Kiongozi huyo wa zamani wa Uganda aliyepinduliwa mwaka 1979, alifariki dunia Agosti 16, 2003 katika Hospitali ya King Faisal mjini Jeddah, Saudi Arabia, na kuzikwa huko huko nchini Saudi Arabia.

Pia, yupo Mobutu Sesseseko ambaye alikuwa rais wa Zaire ambayo sasa ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya kuchukua uongozi kupitia mapinduzi ya 1965.

Mobutu alitawala nchi hiyo kwa kipindi cha miaka 32 kabla ya kuondolewa madarakani kupitia uasi wa mwaka 1997.

Alikimbilia mjini Rabat, nchini Morocco mwezi Mei 1997, kabla ya kufariki kwake, Septemba 7, 1997 kwa saratani ya tezi dume akiwa na umri wa miaka 66, na kuzikwa huko huko.

Ahmadou Babatoura Ahidjo alikuwa rais wa kwanza wa Cameroon kutoka 1960 hadi 1982 alipojiuzulu. Mwaka 1884 alishutumiwa kula njama ya mapinduzi dhidi ya Biya.Ahidjo alihukumiwa kifo bila kuwepo, lakini alikufa 1989 akiwa uhamishoni huko Dakar, Senegal na akazikwa huko huko. 

Hissen Habré, alikuwa rais wa tano wa Chad kutoka 1982 hadi alipoondolewa madarakani 1990. Utawala wake uligubikwa na dhuluma za kikatili dhidi ya wapinzani, ikiwa ni pamoja na madai ya kuteswa na kuuawa kwa wapinzani. Habre ambaye alifariki kwa ugonjwa wa Uviko 19, akiwa na umri wa miaka 79 na kuzikwa jijini Dakar nchini Senegal.

Rais wa zamani wa Tunisia Zine El Abidine Ben aliongoza nchi hiyo kati ya mwaka 1987 na 2011, kabla ya kuondoka madarakani Januari 2011 huku kukiwa na wimbi kubwa la maandamano mitaani.Alikimbilia Saudi Arabia ambapo alifariki Septemba 2019 akiwa na umri wa miaka 83.

Alizikwa katika mji wa Medina, Saudi Arabia.

Shujaa wa Ghana Kwame Nkrumah, alifariki Aprili 27, 1972 nchini Romania alipokuwa akipokea matibabu

Alikuwa waziri mkuu wa kwanza Mwafrika wa Ghana, ambaye atakumbukwa kwa kuiongoza Ghana kupata uhuru wake mwaka 1957 kabla ya kupinduliwa mwaka 1966.

Baada ya kifo chake kilichotokea Aprili 1972, aliyekuwa kiongozi wa Guinea-Conakry, Sekou Toure alisisitiza kuwa ni lazima Nkurumah azikwe nchini humo, kwani alikuwa amepewa hadhi ya kuwa rais wa mwenza wa Jamhuri ya Guinea mwaka 1966 wakati alipopinduliwa Ghana. 

Miezi mitatu baadaye, mabaki ya Nkurumah yalirudishwa na kuzikwa nchin Ghana.

Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us