ULIMWENGU
2 DK KUSOMA
WFP: Nafaka kutoka Ukraine za wasili Kenya chini ya mpango wa Bahari Nyeusi
Umoja wa Mataifa unasema mpango huo umewezesha tani milioni 25 za nafaka na vyakula kusafirishwa katika sehemu tofauti Duniani.
WFP: Nafaka kutoka Ukraine za wasili Kenya chini ya mpango wa Bahari Nyeusi
Grain Deal / Photo: AA
28 Machi 2023

By Coletta Wanjohi

Shirika la Umoja wa mataifa ya mpango wa chakula Duniani , WFP, linasema nafaka iliyonunuliwa kupitia mpango wa Bahari Nyeusi imewasili nchini Kenya kutoka Ukraine.

Mkataba huu kati ya Urusi na Ukaraine unaungwa mkono na Umoja wa Mataifa, na umesimamiwa na Uturuki, Julai 2022, kwa ajili wa kuruhusu usafirishaji salama wa nafaka, vyakula vingine na mbolea, kutoka bandari tatu za Ukraine, licha ya mzozo unaoendela kati ya Urusi na Ukraine.

“Nafaka kutoka kwa wakulima wa ukraine imefika, ambayo inaelekezwa kwa familia zilizo athiriwa na ukame uliokithiri na kulazimika kuhama makaazi yao," WFP inasema katika mtandao wake wa twitter

Tani za metriki 25,000 ni shehena ya kwanza ya Kenya chini ya mpango wa WFP wa kununua chakula kwa nchi zinazo hitaji msaada wa kibinadamu kupitia mpango wa Bahari Nyeusi.

Umoja wa Mataifa unasema Wakenya milioni nne na laki nne wanakabiliwa na njaa kali katika maeneo ya nchi kwa sababu ya ukame wa muda mrefu.

Inaonya kwamba idadi hii inaweza kuongezeka hadi milioni tano na laki nne ifikapo Juni.

WFP imenunua zaidi ya tani 500,000 za ngano kutoka Ukraine chini ya mpango huo.

Ethiopia pia imenufaika kupitia ununuzi wa WFP.

Tarehe 18 Machi 2022, Umoja wa Mataifa ulitangaza kuendeleza mpango wa Bahari Nyeusi. Urusi ilisema iko tayari kurefusha mkataba huo kwa siku 60 zaidi.

Umoja wa Mataifa unatambua jukumu la Serikali ya Türkiye kwa msaada wake wa kidiplomasia na kiutendaji kwa mpango huo.

CHANZO:TRT Afrika
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us