ULIMWENGU
1 DK KUSOMA
Urusi yaporomosha kombora lililorushwa kutoka Ukraine kupiga Crimea
Mzozo kati ya Urusi na Ukraine unaendelea katika siku yake ya 409.
Urusi yaporomosha kombora lililorushwa kutoka Ukraine kupiga Crimea
Makombora ya Ukraine / Others
8 Aprili 2023

Kombora lililorushwa kutoka Ukraine limedunguliwa kwenye Bahari Nyeusi katika mji wa Feodosia huko Crimea eneo linalo dhibitiwa na Urusi, mkuu wa utawala wa Crimea wa Urusi Sergei Aksyonov alisema kupitia mtandao wa Telegram.

Shirika la habari la TASS la Urusi lilimnukuu mshauri wa Aksyonov, Oleg Kryuchkov, akisema kuwa vifusi vimeanguka katika mji wa Crimea, lakini hakuna uharibifu au hasara iliyoripotiwa.

Shirika la habari la Reuters halikuweza kuthibitisha mara moja ripoti za eneo linalotajwa kuwa uwanja wa vita.

Urusi ilitwaa eneo la rasi ya Crimea kutoka kwa Ukraine mwaka 2014. Kiev imeitaka Moscow iirejeshee rasi hiyo.

CHANZO:TRT World
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us