AFRIKA
1 dk kusoma
Rwanda yasitisha kwa muda utoaji wa leseni za biashara ya madini
Bodi ya Madini, Petroli na Gesi ya nchini Rwanda (RMB) imeazimia kuboresha kanuni mbalimbali za sekta hiyo.
Rwanda yasitisha kwa muda utoaji wa leseni za biashara ya madini
Rwanda imesimamisha leseni ya biashara ya madini / Picha: Reuters
25 Juni 2025

Serikali ya Rwanda imesimamisha utaoaji leseni wa biashara ya madini.

Kulingana na bodi ya Madini, Petroli na Gesi nchini humo (RMB), hatua hiyo inatoa nafasi kwa ajili ya uboreshaji wa kanuni za sekta hiyo.

Katika taarifa yake ya Juni 24, 2025, bodi hiyo imesisitiza kuwa uamuzi huo unalenga kuruhusu upitiwaji wa maboresho yenye kusimamia sekta ya madini nchini humo.

Hata hivyo, mdhibiti huyo, hakuweka wazi usitishwaji huo utadumu kwa muda gani, zaidi ya kusisitiza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za kuongeza uwazi, ufanisi katika biashara hiyo nchini Rwanda.

Rwanda inazalisha madini pamoja na bati, tantalamu, tungsten na dhahabu.

 

CHANZO:TRT Afrika and agencies
Kionjo cha TRT Global. Tupe mrejesho wako.
Contact us